Kaunti ya Embu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kaunti ya Embu
Kaunti
Embu monument.jpg
Sanamu iliyo kati mwa mji wa Embu
Embu County Government logo.png
Nembo ya Serikali
Embu County in Kenya.svgEmbu County in Kenya.svg
Kaunti ya Embu katika Kenya
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
Namba14
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuEmbu
GavanaMartin Nyaga Wambora
Naibu wa GavanaDavid Njeru Kariuki
SenetaPeter Njeru Ndwiga
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Jane Wanjuki Njiru
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Embu
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa20
MahakamaMahakama Kuu, Embu
Maeneo bunge/Kaunti ndogo4
Eneo2,555.9 km2 (986.8 sq mi)
Idadi ya watu516,212
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutiembu.go.ke

Kaunti ya Embu ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Makao makuu yako Embu.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Embu inapakana na kaunti za Tharaka Nithi (kaskazini), Machakos (kusini), Kitui (mashariki) na Kirinyaga (magharibi). Sehemu ya Mbeere hujumlisha 74% ya kaunti na ni kavu kuliko sehemu zingine. Sehemu nyingi za kaunti hupata mvua ya kiwango cha mm 500[1].

Mto Tana hupitia katika kaunti hii, upande wa kusini na mashariki katika mpaka na kaunti za Machakos na Kitui. Sehemu hii ya Mto Tana huwa na malambo ya uzalishaji umememaji, yanayojulikana kama Seven Forks Dams.

Mbuga zilizo katika kaunti hiii ni sehemu ya Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Kenya na Hifadhi ya Kitaifa ya Mwea inayopakana na Bwawa la Kamburu[3].

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Embu imegawanywa katika maeneo yafuatayo:

Eneo bunge Wadi
Manyatta Ruguru/Ngandori, Kithimu, Nginda, Mbeti North, Kirimari, Gaturi South
Runyenjes Gaturi North, Kagaari South, Kagaari North, Central Ward, Kyeni Nort, Kyeni South
Mbeere Kusini Mwea, Amakim, Mbeti South, Mavuria, Kiambere
Mbeere Kaskazini Nthawa, Muminji, Evurore

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Fausta Mbura Njiru. Hydrological information for dam site selection by integrating geographic information system GIS and analytical hierarchical process AHP. Iliwekwa mnamo 2018-04-16.
  2. HYDRO POWER STATIONS. Iliwekwa mnamo 2018-04-16.[dead link]
  3. Mwea National Reserve. Iliwekwa mnamo 2018-04-16.