Nenda kwa yaliyomo

Eneo bunge la Mbeere Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi

Eneo bunge la Mbeere Kaskazini (awali: Siakago) ni Jimbo la Uchaguzi nchini Kenya. Ni moja kati ya majimbo mane yaliyo katika Kaunti ya Embu. Jimbo hilo lina wodi tano na zote huwachagua madiwani kwa baraza la Mbeere County.

Mji wa Siakago ambao ni mji mkuu wa Wilaya ya Mbeere unapatikana katika kata ya Nthawa katika jimbo hili.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Jimbo hili lilianzishwa wakati wa uchaguzi mkuu wa 1988 wakati jimbo la Embu Mashariki liligawanywa kutengeneza Jimbo la Runyenjes na Siakago.

Silvester Mate, Mbunge wa kwanza wa Siakago, ndiye alikuwa pia mbunge wa mwisho wa Embu Mashariki baada ya kushinda kiti hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu a 1983[1].

Uchaguzi Mbunge [1] Chama Vidokezo
1988Silvester MateKANUMfumo wa Chama Kimoja
1992Gerald Ireri NdwigaKNCNdwiga alihamuia KANU mnamo 1995 na kushinda uchaguzi mdogo uliofuatia
1997Silas M’Njamiu ItaDPIta aliaga dunia mnamo 1999 [2]
1999Justin Bedan Njoka MuturiKANUUchaguzi Mdogo
2002Justin Bedan Njoka MuturiNARC
2007Kivuti MaxwellSafina

Kata na Wodi

[hariri | hariri chanzo]
Kata
Kata Idadi ya Watu*
Gituburi8,005
Ishiara13,575
Kanyuambora11,658
Kiangombe8,294
Muminji8,390
Mutitu7,040
Ndurumori9,750
Nthawa16,892
Jumlax
*Hesabu ya 1999.
Wodi
Wodi Wapiga Kura
Waliojisajili
Ishiara4,685
Kanyuambora4,812
Kiang'ombe6,844
Muminji5,883
Nthawa9,808
Jumla32,032
*Septemba 2005 [3].

Tazama Pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1 2 Center for Multiparty Democracy: Politics and Parliamenterians in Kenya 1944-2007 Ilihifadhiwa 28 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.
  2. ↑ Daily Nation, 22 Aprili 1999: Siakago MP dies in hospital
  3. ↑ Electoral Commission of Kenya: Registered voters per polling station by electoral area/ward and constituency

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]