Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 2007

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi


Uchaguzi wa Rais 2007[hariri | hariri chanzo]

Uchaguzi wa rais nchini Kenya ulikuwa na matatizo mengi na kusababisha kipindi cha mvurugo na vifo.

Baada ya Raila Odinga wa ODM kuongoza katika hesabu ya kura kwa muda mrefu Tume ya Uchaguzi ya Kenya lilisimamisha hesabu ya kura kwa muda wa usiku mmoja na baada kuanza upya kura za Mwai Kibaki wa PNU zilikuwa mbele. Tume ikamtangaza Kibaki kuwa mshindi aliyeapishwa mara moja bila kusubiri muda wa kisheria kwa malalamiko. Watazamaji waliona kasoro, makosa na matokeo yaliyodokeza ya kwamba hesabu ya kura ilibadilishwa kwenye ngazi za kupiga jumla za kura kimkoa na kitaifa. Vilevile kuna madokezo ya kwamba kura za kiraisi ziliongezwa katika usiku ambako hesabu ilisimamishwa.

Matokeo yaliyotangazwa ni kama yafuatayo:

Wagombea wengine walimaliza kwa kura chache tu.

Uchaguzi wa Bunge 2007[hariri | hariri chanzo]

Tazama Uchaguzi wa Bunge la Kenya 2007 kwa matokeo ya kila jimbo

Wabunge 207 walichaguliwa. Kura zitarudiwa katika majimbo 3. Wabunge 12 wa ziada watateuliwa na rais. Akifuata kawaida atawateua kufuatana na nguvu ya vyama bungeni.

  • PNU na vyama vinavyoshirikishwa nayo vina viti 78 (PNU 43, KANU 16, vyama vingine 21)
  • ODM na chama shirikishwa cha NARC vina viti 102 (ODM pekee 99).
  • ODM-Kenya ina viti 16.
  • Wabunge 11 walichaguliwa kwa majina ya vyama vidogo visivyoshirikishwa na vyama vikubwa.

Magazeti yalitoa taarifa ya kwamba wabunge 30 wa vyama vidogo waliunda "Kundi la vyama vidogo bungeni" (Small Parties Parliamentary Group); idadi hii ingejumlihsa wabunge waliohesabiwa juu kama kundi la PNU.

ODM NARC
ilishirikishwa na ODM
PNU Vyama shirikishwa vya PNU
KANU
Chama chirikishwa na PNU
ODM-Kenya Wabunge wanaojitegemea JUMLA
Wabunge 99 3 43 21 14 16 11 207(of 210)
Vyama shirikishwa vya PNU- KANU (14), Sisi Kwa Sisi (2), Safina (5), NARC-Kenya (4), FORD-Kenya (1), Ford-P (3), New Ford-K (2), Mazingira Party (1), Ford-A (1), DP (2)
Wabunge wa kujitegemea waliingia kupitia vyama vidogo kama PDP (1), PPK (1), NLP (1), KADDU (1), UDM (1), PICK (1), CCU (1), Kenda (1)

Nation 31-12-2007[dead link] Nation 09-01-2008 Archived 16 Januari 2008 at the Wayback Machine.