NARC-Kenya
National Rainbow Coalition–Kenya (NARC-Kenya) ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Kilianzishwa baada ya kushindwa kwa Rasimu ya Katiba inayofadhiliwa na Serikali katika NARC asilia baada ya kura maalumu juu ya katiba ya Kenya 2005.
NARC-Kenya ilipangwa kuwa chama kipya cha kumrudisha Mwai Kibaki kama rais wa Kenya baada ya kuporomoka kwa NARC asilia bila kuacha nembo na jina la "Rainbow".
NARC-Kenya ilikuwa na mafanikio mwaka 2006 katika uchaguzi mdogo ilipopata viti vitatu. Lakini baadaye ilionekana ya kwamba sehemu ya wanaisasa katika serikali ya Kibaki walikataa kuijiunga na chama wakidai athira ya viongozi wa Kenya ya Kati ilikuwa kubwa mno ilikuwa kama umbo tofauti ya Democratic Party of Kenya.
Mnamo Oktoba 2007 miezi michache kabla ya uchaguzi maungano mapya ya Party of National Unity yaliundwa kuwa chombo cha kempeni ya Kibaki.
NARC Kenya 2022
[hariri | hariri chanzo]NARC Kenya ikisimamiwa na Martha Karua ilimuidinisha Kiongozi wa Chungwa Raila Odinga kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa Mwaka 2022.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://www.narckenya.or.ke Archived 15 Agosti 2006 at the Wayback Machine.
- http://www.narckenyausa.org Archived 13 Desemba 2007 at the Wayback Machine.
- Blog kuhusu matatizo ya NARC-Kenya kabla ya kuundwa kwa PNU - tar. 08-10-2007 - imeangaliwa 11.01.2008