Party of National Unity (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Party of National Unity (PNU) au Chama cha Umoja wa Kitaifa ni maungano ya vyama vya kisiasa nchini Kenya yaliyoanzishwa katika Septemba 2007 kabla ya uchaguzi wa rais na bunge. Kusidi lake lilikuwa kuunganisha vikundi vyote vilivyosimama upande wa rais Mwai Kibaki aliyeandaa kugombea urais mara ya pili dhidi ya upinzani wa Orange Democratic Movement (ODM).

Vyama shiriki katika PNU[hariri | hariri chanzo]

Vyama vifuatavyo vilitangazwa kuwa vimeunga mkono katika PNU [1]:

Vyama vingine ambavyo havikutajwa kwenye tovuti rasmi vilishiriki pia kama kwa mfano Ford-Asili, FORD-People na vingine vidogo.

Maandalizi ya chama kipya[hariri | hariri chanzo]

PNU iliundwa haraka inaonekana bila maandalizi mazuri. Hadi mwanzo wa Septemba 2007 haikueleweka Kibaki atagombea urais kupitia chama gani. Chama cha NARC kilichokuwa chombo cha Kibaki mwaka 2002 ilikuwa mkononi mwa mwenyekiti wake Charity Ngilu asiyeonyesha dalili la kumwunga Kibako mkono. Wanasiasa wengi wa upande wa Kibaki waliwahi kuacha NARC na kujenga badala yake NARC-Kenya lakini kikundi hiki hakikujenga uhusiano mzuri na wanasiasa wa serikali ya umoja wa kitaifa walionekana kuwa muhimu kwa Kibaki kama vile Simon Nyachae wa FORD-Kenya au Njenga Karume wa KANU.[1]

Mapatano ya awali[hariri | hariri chanzo]

Hivyo PNU iliundwa katika muda mfupi. Mipango ya awali ilikuwa kumpigania Kibaki kama rais na kuwa na wagombea wa pamoja kwa bunge na ngazi ya miji na tarafa. KANU ilikubaliwa kuwa na wagombea wake wa pekee kwa ajili ya bunge.

Ukosefu wa umoja[hariri | hariri chanzo]

Lakini baadaye vyama vingine vilisisitiza pia kuwa na wabunge wao kwa jina la chama. Kwa hiyo FORD-Kenya, Mazingira, Sisi kwa Sisi na NARC-Kenya vilipeleka wagombea wao mahali pengi pamoja na wagombe katika jina la PNU. Kwa hiyo palikuwa na mashindano mahali mbalimbali kati ya vyama vilivyokubaliana kuwa PNU.

Matokeo ya uchaguzi 2007[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla PNU haikufaulu kupata viti vingi bungeni ni 43 kati ya 210 kulingana na 101 kwa ODM na 15 kwa ODM-K. Viongozi wengi hasa mawaziri wa serikali ya umoja wa kitaifa walishindwa kushika viti bungeni.

Pamoja na vyama vingine vilivyoungana mkono kumpigania Kibaki idadi inaweza kufikia 60-80 kadri matokeo yaliyopatikana hadi 3 Januari 2008. Kwa hiyo PNU itategemea ushirikiano wa vyama vya nje.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]