Nenda kwa yaliyomo

FORD-Asili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ford-Asili)

FORD-Asili (pia: FORD-A) ni chama cha kisisasa nchini Kenya. Jina ni kifupi cha Forum for the Restauration of Democracy-Asili. FORD-Asili ilianzishwa 1992 baada ya farakano ya harakati ya FORD ya pamoja.

Chanzo katika farakano la FORD ya awali

[hariri | hariri chanzo]

FORD (Forum for the Restauration of Democracy) ilikuwa harakati ya kisiasa tangu 1991 iliyopigania kuruhusiwa kwa vyama vingi na demokrasia wakati wa mfumo wa chama kimoja na utawala wa KANU nchini Kenya. Rais Daniel arap Moi alilazimishwa na nchi za nje kukubali uchaguzi wa vyama vingi.

Uchaguzi 1992

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya uchaguzi wa 1992 FORD ilifarakana kati ya wafuasi wa viongozi Kenneth Matiba kutoka Mkoa wa Kati na Martin Shikuku kutoka Mkoa wa Magharibi kwa upande mmoja na kwa upande mwingine Jaramogi Oginga Odinga kutoka Mkoa wa Nyanza. Wafuasi wa Odinga waliunda FORD-Kenya. Wafuasi wa Matiba waliendelea kwa jina la FORD-Asili.

Mgombea wa Ford-A Matiba alipata nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais 1992 kwa asilimia 26.8 za kura baada ya Moi/KANU aliyepata asilimia 36.8. Kutokana na farakano la upinzani Moi alirudishwa kama rais.

Farakano la 1997

[hariri | hariri chanzo]

Chama kiliona matatizo kabla ya uchaguzi wa pili wa vyama vingi 1997. Mwenyekiti Kenneth Matiba na Katibu Mkuu Martin Shikuku walifarakana. Shikuku alishika hati za kusajiliwa kwa chama na Matiba alijiondoa katika siasa hadi kutupa kadi yake ya kupiga kura. Martin Shikuku akawa mgombea wa urais upande wa FORD-Asili.

Wanasiasa wengine waliokaa upande wa Matiba walianzisha chama kipya kwa jina la FORD-People iliyoongozwa na Kimani wa Nyoike.

Mabaki ya Ford-Asili yalipata kura chache tu katika uchaguzi wa 1997 ikashika kiti kimoja tu búngeni.

Uchaguzi 2002

[hariri | hariri chanzo]

2002 Ford-A haikujiunga na harakati ya NARC na kugombea bunge pekee yake. Ilifaulu kushika viti viwili.

Uchaguzi 2007

[hariri | hariri chanzo]

Katika uchaguzi wa 2007 Ford-A ilijiunga na ushirikiano wa PNU wa Mwai Kibaki na kumrudisha mbunge 1 bungeni.