Mkoa wa Magharibi (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mikoa ya Kenya
Mkoa wa Magharibi
Western Province
Mahali pa Mkoa wa Kati
Makao Makuu Kakamega
’‘‘Mji Mkubwa’’’ Kakamega
Eneo

- Jumla
Nafasi ya 7 kati ya mikoa ya Kenya
8,285 km²
Wakazi


 - Jumla (2007)  - Msongamano wa watu / km²
Nafasi ya 5 kati ya mikoa ya Kenya
3,569,400
431/km²
Lugha mkoani Kiluhya

Mkoa wa Magharibi (Western Province) ni mkoa mdogo kati ya mikoa ya Kenya ni pia mkoa mwenye msongamano mkubwa wa watu. Umepakana na Uganda na mikoa ya Kenya ya Nyanza na Bonde la Ufa.

Eneo lake ni 8,285 km² pekee kuna wakazi 3,569,400 hivyo hukaa zaidi ya watu 400 kwa kila kilomita ya mraba. Wakazi wa Magharibi ni hasa Abaluhya (Waluhya). Mji mkuu ni Kakamega.

Nchi ya mkoa limeenea kutoka vilima vya Bungoma mpakani wa Uganda hadi tambarare karibu na Ziwa Viktoria. Mlima mkubwa wa pili wa Kenya ni Mlima Elgon uko ndani ya mkoa kwenye mpaka wa Uganda. Msitu wa Kakamega ni kati ya misitu asilia ya mwisho wa Kenya.

Uti wa mgongo wa uchumi wa mkoa ni kilimo. Pamoja na kilimo cha kujikimu kuna pia mashamba makubwa ya chai na miwa. Kilimo na maliaili ni msingi wa viwanda vikubwa kama vile kiwanda cha sukari cha Mumias au kiwanda cha karatasi cha Webuye. Hata hivyo idadi kubwa ya wakazi ni maskini na wanaume wengi wameenda Nairobi au kwenye hoteli za pwani kwa kazi ya ajira.

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Kuna wilaya nane mkoani:

Wilaya Makao makuu
Bungoma Bungoma
Busia Busia
Butere/Mumias Butere
Kakamega Kakamega
Lugari Lugari
Mlima Elgon Kapsokwony
Teso Malaba
Vihiga Vihiga


 
Mikoa ya Kenya
Bendera ya Kenya
Bonde la Ufa | Kaskazini-Mashariki | Kati | Magharibi | Mashariki | Nairobi | Nyanza | Pwani