Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Mashariki (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikoa ya Kenya
Mkoa wa Mashariki
Eastern Province
Mahali pa Mkoa wa Mashariki
Makao Makuu Embu
’‘‘Mji Mkubwa’’’ Machakos
Eneo

- Jumla
Nafasi ya 2 kati ya mikoa ya Kenya
154,354 km²
Wakazi


 - Jumla (2007)  - Msongamano wa watu / km²
Nafasi ya 2 kati ya mikoa ya Kenya
5,380,200
35/km²
Lugha mkoani Kikamba, Kimeru
lugha za wahamiaji kama Kiturkana
Kiborana

Mkoa wa Mashariki (Eastern Province) ni mkubwa wa pili kati ya mikoa minane ya Kenya. Umepakana na Ethiopia halafu na mikoa ya Bonde la Ufa, Kati, Nairobi, Pwani na Mashariki-Kaskazini.

Eneo la mkoa ni 154,354 km² kuna wakazi karibu milioni tano na nusu. Umbo lake ni kanda ndefu linalounganisha watu wenye maisha na utamaduni tofauti sana. Katika kusini kuna wakulima wanaotumia lugha za Kibantu kama vile Wakamba na Wameru. Maeneo mapana ya kaskazini ni yabisi yakikaliwa na wahamiaji kama Borana, Turkana, Wasomali na wengine. Makao makuu ya mkoa yapo mjini Embu.

Ndani ya mkoa kuna maeneo yenye rutba sana hasa karibu na Mlima Kenya. Sehemu kubwa za Ukambani ni yabisi kiasi na wakulima wake hukosa mvua kila baada ya miaka kadhaa na kuteswa na njaa. Kaskazini ni nchi yabisi hata jangwa kama jangwa la Chalbi kati ya Ziwa Turkana na Marsabit.

Wilaya[hariri | hariri chanzo]

Wilaya - (Makao Makuu)

a Inaitwa piaWilaya ya Nyambene.
b Inaitwa pia Wilaya ya Nithi.