Nenda kwa yaliyomo

Wilaya ya Tharaka

Majiranukta: 0°18′S 38°0′E / 0.300°S 38.000°E / -0.300; 38.000
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Tharaka ilikuwa moja kati ya Wilaya 71 za Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Makao makuu yalikuwa mjini Tharaka (Marimanti).

Kwa sasa imekuwa sehemu ya kaunti ya Tharaka-Nithi.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Wilaya hii ilipatikana katika Mkoa wa Mashariki wa Kenya ikiwa na ukubwa wa ardhi wa km2 1570.

Idadi ya Wakazi

[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya watu katika Wilaya hii kulingana na Hesabu ya 1999 ni 100,992[1], na hakuna wanaohesabiwa kuwa wakazi wa Mtaani. Mnamo 1998, Wilaya hii ilitenganishwa kutoka Tharaka-Nithi[2], ambayo pia ilikuwa sehemu ya Wilaya Kubwa ya Meru.

Tharaka ndiyo maskani ya watu wa Ameru (Wameru) ambao wakati mwingine wanatajwa kuwa na uhusiano na makabila mengine yaishiyo katika maeneo ya Mlima Kenya: Wakikuyu na Waembu.

Wameru ni Wabantu ambao wameishi kando ya Mlima Kenya kwa miaka mingi, hata kabla ya ukoloni.

Watu wengi wa Tharaka ni wa dini ya Kikristo (Methodist, Presbyterian na Roman Catholic), ikiashiria kazi ya wamisionari.

Wengine ni Wahindi, ambao dini yao ni Hindu.

Pia kuna Waafrika na Waarabu ambao ni Waislamu.

Tharaka pia ina baadhi ya wakazi wa asili ya Ulaya.

Tharaka ilikuwa na baraza moja tu, Tharaka County. Pia Jimbo moja la uchaguzi, Tharaka.

Tarafa za Utawala
Tarafa Idadi ya wakazi* Makao Makuu
Tharaka ya Kati 38,914 Marimanti
Tharaka Kaskazini 36,904 Gatunga
Tharaka Kusini 25,174 Chiakariga
Jumla 100,992 -
* 1999 census. Viini: [1], [2],

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

0°18′S 38°0′E / 0.300°S 38.000°E / -0.300; 38.000

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mashariki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Tharaka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.