Kericho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kericho, Kenya


Kericho
Kericho is located in Kenya
Kericho
Kericho

Mahali pa mji wa Kericho katika Kenya

Majiranukta: 0°22′0″S 35°18′0″E / 0.36667°S 35.30000°E / -0.36667; 35.30000
Nchi Kenya
Kaunti Kericho
Idadi ya wakazi (2009)
 - Wakazi kwa ujumla 103,911

Kericho ni mji wa Kenya ya kusini magharibi na makao makuu ya kaunti ya Kericho katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki wenye wakazi 42,029 ambao pamoja na vitongoji wa nje hufikia 104,282 kwa eneo kubwa la mji[1].

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kimo cha Kericho kutoka usawa wa bahari ni mita 2,070. Ni kitovu cha eneo la mashamba ya chai. Makampuni makubwa ya chai yana ofisi mjini. Chai inayokuzwa Kericho ni mashuhuru kwa ladha yake nzuri na rangi ya kuvutia. Pia wilaya hii ina wanariadha wa kukimbia mbio za mbali wa hali ya juu sana ambao mara kwa mara wanashinda medali za dhahabu katika mashindano mbalimbali.

Chanzo cha maji cha msitu mau ambacho ni kikubwa kuliko zote nchini Kenya kinapatikana mjini Kericho. Mji huu ni makao makuu ya sekta kubwa ya kilimo cha chai nchini Kenya. Makampuni makubwa ya chai kwa mfano Unilever Kenya' James Finlay na Williamson tea zinapatikana hapa. Chai inayokuzwa hapa huwa inasafirishwa na kuuzwa nchi za Uropa hasa Uingereza. Idadi ya watu wote kwenye kaunti hii ni 752,396 (sensa 2009).

Msitu huko Kericho.

Historia na Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Kericho ni kitovu cha kilimo cha chai nchini Kenya.

Eneo la mji hukaliwa kiasili ya Wakipsigis ambao ni sehemu ya Wakalenjin. Jamii ya wakipsigis wanasifika kuwa watu walioshika mila zao na pia watu wakarimu. Wanariadha wengi mashuhuri kwa mfano Kipchoge Keino wametoka katika jamii hii.

Chakula mashuhuri cha jamii hii ni kimyet(Ugali) ambayo inaliwa pamoja na mboga za majani, mursik(maziwa ya mgando) na nyama. Chai pia inanywewa sana katika jamii hii, hasa asubuhi na baada ya kula.

Jina la mjii huu linasemekana kwamba linatokana na mganga wa zamani wa Kikipsigis aliyeitwa Kipkerich.

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Usafiri unaotumiwa sana ni wa magari. Barabara za wilaya hii zipo katika hali nzuri ukilinganisha na wilaya zingine nyingi za nchini Kenya. Barabara kuu tatu zinaelekea mjini Kericho, barabara ya Kisumu-Kericho, barabara ya Kisii-Kericho na barabara ya Nakuru-Kericho. Mabasi na matatu yanatumiwa kwenda miji mingine.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]