Nenda kwa yaliyomo

Kipchoge Keino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kipchoge Keino 2014

Kipchoge ("Kip") Keino ni Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Kenya na mkimbiaji aliyestaafu akiwa na ushindi wa medali za dhahabu mara mbili kwenye Mashindano ya Olimpiki. Alizaliwa 17 Januari 1940 huko Kipsamo, Wilaya ya Nandi, Kenya.

Alianza kuonyesha ufundi wake wa kukimbia kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola huko Perth, Australia alipochukua nafasi ya kumi na moja. Kwenye Mashindano ya Olimpiki ya Majira ya Joto mwaka 1964 alimaliza wa tano kwenye mbio za mita 5000.

27 Agosti 1965, Keino alivunja rekodi ya dunia ya mita 3000 kwa sekunde sita. Katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika mwaka..........alishinda medali mbili za dhahabu kwa umbali wa mita 1500 na 5000. Baadaye alikuja kuvunja rekodi ya dunia iliyokuwa ikishikiliwa na Ron Clarke ya mita 5000 kwa kukimbia kwa muda wa 13:24:2.

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Kipchoge Keino kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.