Kaunti ya Machakos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ili kusoma kuhusu mji, soma Machakos

Kaunti ya Machakos
Kaunti
Office of the Governor, Machakos County.jpg
Ofisi ya gavana wa Machakos
Flag of Machakos County.png
Bendera
Machakos County in Kenya.svgMachakos County in Kenya.svg
Kaunti ya Machakos katika Kenya
Coordinates: 01°14′S 37°23′E / 1.233°S 37.383°E / -1.233; 37.383
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
Namba16
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Mashariki
Makao MakuuMachakos
Miji mingineKangudo, Matuu, Kithimani, Athi River
GavanaDkt. Alfred Mutua, CBS
Naibu wa GavanaENG. Francis Maliti Wambua
SenetaBoniface Mutinda Kabaka
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Joyce Kamene
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Machakos
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa40
Maeneo bunge/Kaunti ndogo8
Eneo5,952.9 km2 (2,298.4 sq mi)
Idadi ya watu1,098,584
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutihttp://www.machakosgovernment.com/

Kaunti ya Machakos ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Makao makuu yako Machakos. Inatarajiwa kuwa na mji wa Konza ambao ndio mji wa kwanza wa teknohama katika Afrika Mashariki.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Machakos inapakana na Nairobi, Kiambu, Murang'a (magharibi), Embu (Kaskazini), Kitui (mashariki), Makueni na Kajiado(kusini). Tabianchi ya Kaunti ya Machakos ni nusu kavu. Ina mandhari yenye vilima[1]. Udongo katika maeneo mengi ni udongo wa mfinyanzi ulio mwekundu. Hata hivyo, kuna mito ambayo huchimbwa mchanga haramu. Jambo hili huharibu mandhari kwa kukausha mito[2].

Mto Tana na Mto Athi hupitia katika kaunti hii. Bwawa la Masinga liko kaskazini katika mpaka wa Machakos na Embu.

Kiwango cha ardhi kilicho misitu ni 7.6%. Vyanzo vya maji katika kaunti ni Vilima vya Iveti, Muumandu, Kalimanzalu and Kiima Kimwe[2].

Machakos hupata misimu miwili ya mvua, Oktoba hadi Disemba na Machi hadi Mei. Maeneo yaliyo na vilima hupata mvua mingi, kiwango cha mm 1000, kuliko maeneo kavu ambayo hupata mvua ya kiwango cha mm 500. Mwezi wa Julai huwa na baridi zaidi[2].

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Machakos imegawanywa katika maeneo yafuatayo[3]:

Eneo bunge Wadi
Masinga Kivaa, Masinga, Central, Ekalakala, Muthesya, ndithini
Yatta Ndalani, Matuu, Kithimani, Ikomba, Katangi
Kangundo Kangundo North, Kangundo Central, Kangundo East, Kangundo West
Matungulu Tala, Matungulu North, Matungulu East, Matungulu West, Kyeleni
Kathiani Mitaboni, Kathiani Central, Upper Kaewa/Iveti, Lower Kaewa/Kaani
Mavoko Athi River, Kinanie, Muthwani, Syokimau/Mulolongo
Machakos Town Kalama, Mua, Mutitini, Machakos Central, Mumbuni North, Muvuti/Kiima-Kimwe, Kola
Mwala Mbiuni, Makutano/Mwala, Masii, Muthetheni, Wamunyu, Kibauni

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Machakos Government - Official Website. Iliwekwa mnamo 2018-04-18.
  2. 2.0 2.1 2.2 Machakos County Integrated Development Plan, 2015. Iliwekwa mnamo 2018-04-26.
  3. Machakos County. Iliwekwa mnamo 2018-04-18.