Tana (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Tana)
Chanzo cha Tana (picha kutoka angani).
Mto Tana mwaka 1998 wakati wa El Nino.
Mto Tana mwaka 1998 wakati wa El Nino.

Tana ni jina la mto mrefu kuliko yote ya Kenya ukiwa na urefu wa takriban km 650.

Chanzo chake ni milima ya Aberdare magharibi kwa Nyeri. Mwanzoni unelekea mashariki, halafu inapinda kuzunguka Mlima Kenya upande wa kusini. Kisha huingia ndani ya mabwawa ya Masinga na Kiambere yaliyotokana na bwawa la Kindaruma. Chini ya bwawa mto huu hugeuka kuelekea kaskazini na kutiririka mpaka wa kaskazini-kusini kati ya kaunti za Meru na Kitui, Bisanadi, Kora na Hifadhi ya wanyama ya Rabole. Ndani ya hifadhi hugeuka kuelekea mashariki, na kisha kusini mashariki.

Kati ya mito inayoingia mto wa Tana kuna mto Thika.

Inapita miji ya Garissa, Hola na Garsen kabla ya kufika Bahari Hindi kwenye Ghuba ya Ungwana.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]