Lango:Kenya
Lango hili lipo katika ujenzi
Milango ya Wikipedia: Sanaa · Utamaduni · Jiografia · Afya · Historia · Hisabati · Sayansi · Falsafa · Dini · Jamii · Teknolojia WikiLango KenyaJamhuri ya Kenya ni nchi iliyoko Afrika Mashariki katika ikweta, kando ya Bahari ya Hindi. Kenya imepakana na Ethiopia (kaskazini), Somalia (kaskazini mashariki), Tanzania (kusini), Uganda na Ziwa Victoria (magharibi), kisha Sudan Kusini (kaskazini magharibi). Mji mkuu ni Nairobi. Mji mkuu ni Nairobi. Idadi ya watu imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni na kufikia milioni 50. Kenya ina mbuga mbalimbali wanamoishi maelfu ya wanyama pori wa kila aina. Jina Kenya linatokana na mlima Kenya, ulio wa pili kwa urefu barani Afrika, Kabla ya mwaka wa 1920, eneo linaloitwa Kenya liliitwa Himaya ya Uingereza Afrika Mashariki, kwa hivyo hapakuwa na haja kutaja neno mlima uliporejelea mlima huo. Makala iliyochuguliwaNairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mmojawapo wa mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Afrika. Kulingana na sensa ya 2009, Nairobi ina wakaaji 3,138,295. Pamoja na vitongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Afrika. Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkare nairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi." Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi, lakini hasa Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng. (Soma zaidi...) Picha iliyochaguliwaJe wajua ...Wasifu uliochaguliwaTom Mboya (15 Agosti, 1930 - 5 Julai, 1969) alikuwa mwanasiasa maarufu Kenya wakati wa serikali ya Mzee Jomo Kenyatta. Yeye pia alianzisha chama cha Nairobi People's Congress Party, chama ambacho kilichangia kukua kwa chama maarufu Kenya African National Union (KANU), alikuwa pia Waziri wa Mipango na Maendeleo ya Uchumi wakati wa kifo chake. Mboya aliuawa tarehe 5 Julai, 1969 katika mji mkuu wa Nairobi. JamiiMasomo inayohusu KenyaMilango inayohusianaAssociated Wikimedia |