Uchumi wa Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Uchumi wa Kenya Kipindi cha Uongozi wa Kenyatta[hariri | hariri chanzo]

Miaka kumi na tano ya Uhuru wa Kenya, kama ilivyokua miaka iliyopelekea uhuru, ilitawaliwa na sifa zilizomhusu Jomo Kenyatta miongoni mwa watu. Utawala wa Kenyatta uliofikia kikoma mnamo Agosti 1978, wakati kitabu hiki hakijakamilika, unaelezewa kwa ufasaha na. Kinaelezea mchango aliokuwanao Rais huyo katika muelekeo wa Kibepari (capitalist) na kijamaa (socialist) unaodhihirika katika mikakati ya kiuchumi nchini Kenya hivi sasa. Ushawishi wa ari ya “kinyakuzi” enzi za Kenyatta ulikuwa na athari zake. Jomo Kenyatta, muasisi wa Taifa la Kenya atakumbukwa daima kwa mchango wake katika kupatikana kwa uhuru nchini mwake. Hata hivyo, inasemekana kuwa uhuru wa Kenya ulikuja na matatizo chungu mzima: Ukabila, Rushwa, na Choyo. Nafasi za kiutawala zilipatikana kwa wachache waliokuwa na madhumuni ya kukusanya Utajiri mkubwa kadiri iwezekanavyo. Hata hivyo, mtizamo huu wa jinsi hali ilivyokuwa, unakingana na jinsi hali halisi ilivyokuwa. Je? Hakukuwa na ukabila kabla ya uhuru? Kiukweli, Jomo Kenyata hakuwa muanzilishi, bali mdhibiti mkuu wa hali ya kikabila nchini humo. Ulikuwepo na bado upo japo kuwa unadhihirika katika ngazi fulani fulani. Miezi ya mwanzo ya utawala wa Rais Daniel Arap Moi, ilitawaliwa na bidii za dhati za kutaka kuondoa makosa yote yaliyojidhihirisha katika utawala uliotangulia na kwa bahati mbaya, ulikuwa ni wakati mbaya na mgumu kiuchumi nchini Kenya. Hata hivyo, mawazo ya kuwa matatizo yote yangeweza kuisha kufumba na kufumbua, yalikosa msingi pamoja na uzuri wa matokeo yaliyokusudiwa na kwamba ukabila na rushwa ambavyo hupatikana ulimwenguni kote, vingeweza kupotea. Ni rahisi sana kulaumu nyakati zilizopita kuwa ni sababu ya matatizo ya sasa na ni rahisi pia kufikiri kuwa mambo mazuri yanaweza kupatikana kwa haraka. Kukubali matatizo yaliyouandama uongozi wa Kenyatta, sio kukataa mazuri yalo ambatana nao. Hatua kubwa zilipigwa kimaendeleo ya jamii ya watu wa Kenya miaka kumi na tano baada ya uhuru, bila kuzingatia baadhi ya maandiko yanayoweza kuwa yameandikwa nchini Kenya na kitabu hiki, kinalenga kutoa ukweli na uhalisia wa mambo.

Kutoka[hariri | hariri chanzo]

  • “The economy of Kenya. The Kenyatta era”, Arthur Hazlewood 1979.