Utalii nchini Kenya
Utalii nchini Kenya ni sekta iliyo chanzo kikuu cha mapato ya fedha za kigeni baada ya kilimo.[1]
Kenya ni kati ya nchi zilizo na mazingira murua zaidi ulimwenguni na bila shaka watalii hufurahia mno kuzuru eneo hili. Kama wahenga walivyosema kuwa kutembea kwingi ni kuyaona mengi, Rabuka ametunukia Kenya hidaya kochokocho kwa kuipatia wanyama wengi, misitu na maskani rembo kupindukia.
Vivutio vikuu vya utalii ni safari za picha kupitia mbuga za kitaifa na michezo ya uhifadhi ambayo idadi yao ni 19. Vivutio vingine ni pamoja na misikiti katika jiji la Mombasa; mandhari inayojulikana ya Bonde la Ufa; shamba la kahawa mjini Thika; mtazamo wa Mlima Kilimanjaro, ukivuka mpaka kuingia Tanzania;[2] na fukwe zake kando ya Bahari ya Hindi. Hata hivyo kuna mapato mengi ya kitalii nchini Kenya .
Historia
[hariri | hariri chanzo]Lee Jolliffe, katika kitabu chake anasema utalii wa Kenya uliendelea kwa kuhifadhi maliasili, ingawa "utalii wa fukwe, utalii ya eco, utalii wa utamaduni na utalii wa michezo zote zinafomu sehemu moja." [3]
Katika miaka ya 1990, idadi ya watalii waliokuwa wakisafiri nchini Kenya ilipungua kwa sababu ya mauaji ya watalii.[4] Hata hivyo, utalii nchini Kenya umekuwa chanzo kinachoongoza cha mapato ya fedha za kigeni tangu mwaka 1997, wakati uliupita kahawa, na mwenendo uliendelea, isipokuwa miaka 1997-1998.[3]
Mgogoro wa Kenya wa 2007-2008
[hariri | hariri chanzo]Kufuatia uchaguzi wa urais wa mwaka wa 2007 na mgogoro wa Kenya 2007-2008 uliofuata, mapato ya utalii ulitimazi kutoka asilimia 54 mwaka 2007 katika robo ya kwanza ya 2008.[1] Mapato yalishuka hadi shilingi bilioni 8.08 (dola milioni 130.5 za Amerika) kutoka shilingi bilioni 17.5 katika miezi ya Januari hadi Machi 2007 [1] na jumla ya watalii 130,585 waliwasili nchini Kenya ikilinganishwa na watalii 273,000 na mwaka huo.[5] Mapato ya Watalii kutoka Uchina, hata hivyo, ilishuka aslimia 10.7, ikilinganishwa na zaidi ya asilimia 50 kutoka mapato ya jadi ambao ni Marekani na Ulaya.[1] Utalii wa ndani pia uliboreshwa kwa asilimia 45, kuichuma sekta ya utalii shilingi bilioni 3.65 juu ya bilioni 8.08 kwa kipindi ambacho kilikuwa kinapitiwa.[5]
Utalii wa Mkutano ulisambaratika wakati wa robo ya kwanza kwa kuanguka kwa asilimia 87.4 ikilinganishwa na ongezeko lililoshuhudiwa mwaka wa 2007.[5] Watu 974 waliowasili nchini Kenya katika kipindi hicho kwa ajili ya mikutano waligundua kuwa mikutano hiyo ilikuwa imefutiliwa mbali.[5] Biashara ya Kusafiri ilipungua kwa asilimia 21 wakati wa kipindi hicho na wasafiri 35,914 walikuja nchini ikilinganishwa na 45,338 katika kipindi kama hicho mwaka kabla.[5]
Licha ya hayo, Kenya ilishinda tuzo la Best Leisure Destination katika ramsa ya World Travel mjini Shanghai, China, mwezi Aprili 2008.[6] Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii nchini Kenya, Rebecca Nabutola, alisema kwamba "tuzo hili ni ushuhuda kwamba Kenya ina bidhaa ya kipekee ulimwenguni ambayo ni utalii. Kutambuliwa kwa Kenya bila shaka kutainua utalii wa Kenya na kuongeza utambulisho wake kama sehemu inayoongoza ya kitalii.[6]
Vivutio vya wageni
[hariri | hariri chanzo]Mbuga za Kitaifa
[hariri | hariri chanzo]Kenya imeorodheshwa miongoni mwa nchi zinazoongoza katika sekta ya wanyamapori zaidi ya miaka arobaini na inajulikana kote ulimwengu kwa ajili yake. Kuna hifadhi za taifa, mapori ya akiba na ya wanyama na kuonekana wakati mwingine havina uhai kimya na hata hivyo kuna wanyamapori wengi mno. Mashimo ya maji na mabwawa ni muhimu ambapo wanyama wanaweza kunywa maji ili kukata kiu.
Hifadhi ya taifa ya Amboseli
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya Taifa ya Amboseli, ambayo zamani ilikuwa inaitwa hifadhi ya wanyama ya Maasai Amboseli, iko katika Wilaya ya Kajiado, Mkoa wa Bonde la Ufa, nchini Kenya. Mbuga hii ina ukubwa wa eneo wa kilomita 390 katika msingi wa eneo la kilomita 8,000 na inaenea mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Wenyeji wa sehemu hii ni Wamasai, lakini watu kutoka maeneo mengine ya nchi wanakaa huko kwani walivutiwa na uchumi uliofanikiwa na ambao ulisababishwa na utalii na kilimo kabambe kandokando ya mifumo wa mabwawa ambayo yanaifanya eneo hili lenye mvua kidogo (wastani wa milimita 350 kwa mwaka) kuwa mojawapo ya sehemu bora duniani kuwatazama wanyamapori. Mbuga hii hulinda mabwawa mawili kwa matano ambayo yako, na inahusisha ziwa lililokauka la Pleistocene na mimea yenye nusu-ukame.
Mbuga ya kitaifa ya Kora
[hariri | hariri chanzo]Mbuga ya kimataifa ya Kora iko Mkoani Pwani, Kenya. Mbuga hii ina upana wa eneo a eneo wa kilomita 1787. Mbuga hii imejasisiwa kilomita 125 mashariki mwa Mlima Kenya. Awali mbuga hii ilijaridiwa kama hifadhi ya kiasili mwaka wa 1973. Ilijaridiwa kama mbuga ya kitaifa mwaka wa 1990, kufuatia mauaji ya George Adamson na wawindaji wanyama.
Mbuga ya kitaifa ya Ziwa Nakuru
[hariri | hariri chanzo]Mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Ziwa Nakuru, lililoanzishwa mwaka wa 1961 karibu na Ziwa Nakuru, liko karibu na mji wa Nakuru. Inajulikana sana kwa maelfu, na wakati mwingine mamilioni ya ndege wa aina ya flamingo wanaokusanyika ufuoni mwa ziwa Nakuru. Wajihi wa ukame wa ziwa hili ni vigumu kujulikana kwa sababu ya flamingo wengi. Idadi ya flamingo katika ziwa hutegemea maji na hali ya chakula. Pahali bora kuwatazama ndege hawa ni juu ya mwinuko unaoitwa Baboon Cliff.
Kivutio kingine ni eneo la kilomita 188 lililo kandokando ya ziwa hilo na limezingirwa na ukuta kuwalinda wanyama walio katika hatari ya kukoma kama twiga wa Rothschild na vifaru weusi.
Mbuga ya Taifa ya Mlima Kenya
[hariri | hariri chanzo]Mbuga ya taifa ya Mlima Kenya 0°07′26″S 37°20′12″E / 0.12389°S 37.33667°E, iliyoanzisha mwaka wa 1949, hulinda kanda inayozunguka Mlima Kenya. Awali ilikuwa ni hifadhi ya misitu kabla ya kutangazwa kama mbuga ya kitaifa. Hivi sasa ni mbuga ya taifa ndani ya hifadhi ya misitu ambayo imeizunguka.[7]Mnamo Aprili mwaka wa 1978 eneo hilo lilifanywa hifadhi la Biosphere la UNESCO. [8] Mbuga ya taifa na hifadhi ya misitu ziliunganishwa zikawa katika orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO mwaka wa 1997.[9]
Mbuga ya Taifa ya Nairobi
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya taifa ya Nairobi ilikuwa mbuga ya kwanza nchini Kenya ilipoanzishwa mwaka wa 1946. Iko takriban kilomita 7 kusini mwa katikati ya Nairobi, mji mkuu wa Kenya, na ni ndogo ikilinganishwa na mbuga nyingine za wanyama barani Afrika. Majumba marefu jijini Nairobi yaweza kuonekana kutoka kwenye mbuga.
Mbuga hii ina wanyamapori wengi tofauti.[10] Ni ugo tu unaotenganisha mbuga hii ya wanyama kutoka mji mkuu.[11] Wanyama walao mimea hujaa sana katika mbuga hii wakati wa kiangazi. Ni mojawapo kati ya makimbilio ya vifaru yaliyofanikiwa sana nchini Kenya.
Kwamba mbuga hii ipo karibu na jiji la Nairobi husababisha mgogoro baina ya wanyama na wananchi na pia hutishia uhamaji wa wanyama.
Hifadhi ya Taifa ya Aberdare
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya Taifa ya Aberdare ina latitudo ya mita 1829 hadi 4001 juu ya usawa wa bahari na iko katika ardhi kati ya kusini-magharibi kwa Mlima Kenya.
Ilianzishwa rasmi mnamo Mei 1950 kama hifadhi ya misitu ya nchi. Hifadhi ina hewa njema iliyo tulivu na yenye mazingira murua na mvua kubwa inayonyesha mwaka nenda mwaka rudi.
Mbuga ya Masai Mara
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya Masai Mara ni mojawapo kati ya maskani bora zaidi ambapo wanyamapori wengi wamehifadhiwa. Hapa ndipo wanapoishi zaidi wanyama wenye kutambulika kama ‘watano wakubwa’: simba, chui, ndovu, nyati na kiboko. Hapa watalii hasa watoto hufurahishwa sana na mazingira na maajabu mengi wanayoyaona.
Hifadhi ya Taifa ya Meru
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi hii imekuwa yenye shughuli kabambe na yenye watalii chungu nzima waliofurika furifuri ili kujionea maajabu ya Mlima Kenya. Huku kuna wanyama si haba ambao hutokea misitu iliyokaribia Mlima Kenya. Hapa watalii huzuru ili kuikwea milima na kuipata hewa safi.
Mbuga ya Samburu
[hariri | hariri chanzo]Samburu ni "nchi huru" ambapo Joy Adamson alikasirishwa mno na simba. Hii imeifanya mbuga hii kuwa maarufu sana na kuwafanya watalii wengi kutaka kuizuru.
Watalii pia huvutiwa mno na tamaduni za Wasamburu ambao mavazi na mienendo yao huvutia sana.
Mbuga ya Tsavo Mashariki
[hariri | hariri chanzo]Tsavo Mashariki hujumlisha eneo la kilometamraba 13,747 Mashariki Kusini mwa Kenya. Mazingira murua ndiyo yanayowavutia watu zaidi kuzuru mbuga hii.
Baadhi ya mambo yanayopendeza ni Mto Tana, ufuko wa bahari, makazi ya viboko, hifadhi ya tembo, joto na hali ya anga yenye kupendeza na sehemu nyingine mbalimbali.
Fukwe
[hariri | hariri chanzo]Kenya na Tanzania zina ukanda wa pwani nzuri na mwanga wa jua kwa njia ya nje ya mwaka hata wakati wa mvua. Wengi wa wenyeji kwa kuchukua hiyo fukwe ni tupu isipokuwa kwa mapumziko ya kitaifa katika nchi zote mbili. Hivyo unaweza kutumia muda katika pwani ya umma na kujisikia kama ni saa ya kipekee pwani. Ni pwani ya Kenya na hoteli kadhaa kwamba mtu anaweza kuchagua.
Matembezi nchini Kenya
[hariri | hariri chanzo]Matembezi nchini Kenya ni ya kufana kwa na huwavutia watalii chungu nzima kila mwaka. Matembezi hayo yapo katika mji wa Nairobi njia ya Lang’ata karibu na malazi ya wanyama ya Nairobi. Katika matembezi hayo utaweza kujionea mengi kwani kutembea kwingi ni kuona mengi, pia utaweza kuushuhudia utamaduni wa Wakenya ulionata kama gundi na kuyaona mazingira mema yenye kufana.
Utamaduni wa Wakenya
[hariri | hariri chanzo]Jamii ya Wamasai ni baadhi ya makabila zinazofuata mno tamaduni na asili zao za jadi. Mabadiliko ya kizazi na pengo katika utamaduni bado zinaathiri mitindo ya maisha. Hata hivyo jamii ya Wamasai imejua bayana kwamba mwacha mila ni mtumwa na hivyo kuhifadhi tamaduni zao kupitia mavazi ambayo ni vikoi na leso na viatu vya jadi, maisha yao ambayo ni ya ufugaji wa ng’ombe na lugha yao ya Kimasai.
Wakikuyu nao hawajaachwa nyuma katika kuhifadhi na kukumbatia tamaduni zao ambapo siku baada ya nyingine wao hunywa mvinyo wao wa jadi aina ya karubu, huwatafutia binti zao wachumba na kuwatahiri vijana wao kwa karamu zenye raha na bashasha tele.
Hoteli
[hariri | hariri chanzo]Kuna hoteli mbalimbali za kufana mno ambazo huwa na hali tofauti katika mazingira na hata kwenye fulusi utakazotumia kugharamia ada yako. Baadhi ya hoteli zenye sifa tele ni Intecontinental, Hilton, Winsor, Safari Park na Norfolk zilizo katika mji wa Nairobi. Hapa maliponi ya kiasi cha juu lakini huduma yao ni ya hali ya juu sana
Nakuru na Mombasa pia kuna hoteli za kufana ambapo vyakula vya asili na vile vya kisasa pia hupikwa. Watalii wengi hufurahia sana kukaa huku kwa sababu ya bahari na maziwa yaliyoko katika maeneo haya.
Habari ya Watalii
[hariri | hariri chanzo]Watalii katika nchi nyingi wanahitajika kuwa na pasipoti na visa. Watalii hawa hushauriwa kupata chanjo dhidi ya malaria na homa ya manjano.[2]
Bodi ya Utalii ya Kenya, au KTB, ni shirika la serikali ambao hutafutia soko kwa watalii wanaosafiria nchi ya Kenya.[3] Maoni ya sekta ya kibinafsi zinachapishwa na Wizara ya Utalii, ambayo inafanya kazi unyounyo na KNB.[3] Wizara ya Utalii lina jukumu la kushauri KNB na kufungua bodi katika wizara zinazohusiana na aina maalum za utalii.[3]
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka wa 1995, kulikuwa na vitanda 34,211 vya hoteli na kiwango cha kujaza vitanda hivi kilikuwa asilimia 44. Wageni 1,036,628 waliwasili nchini Kenya mwaka wa 2000 risiti za utalii kwa ujumla zilikuwa dola milioni 257. Mwaka huo, serikali ya Marekani ilikadiria wastani wa gharama ya kuishi mjini Nairobi kuwa dola 202 kwa siku, ikilinganishwa na dola 94 hadi dola 144 kwa siku mjini Mombasa, kutegemea na wakati wa mwaka. [2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Post-poll violence halves Kenya Q1 tourism revenues", Reuters, 2008-05-02. Retrieved on 2008-05-04.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 Encyclopedia ya Mataifa
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Jolliffe 2007, p.146
- ↑ Nagle 1999, p.115
- ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Maina, Wangui. "Kenya: Domestic Tourists Help to Cushion Travel Sector", Business Daily, AllAfrica.com, 2008-05-05. Retrieved on 2008-05-05.
- ↑ 6.0 6.1 Gachenge, Beatrice. "Kenya: Country Scoops Top Tourism Award", Business Daily, AllAfrica.com, 2008-04-21. Retrieved on 2008-05-04.
- ↑ Kenya Wildlife Service (2007). "Mount Kenya National Park". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-22. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.
- ↑ United Nations Environment Programme (1998). "Protected Areas and World Heritage". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-12. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.
- ↑ United Nations (2008). "Mount Kenya National Park/Natural Forest". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-30. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.
- ↑ Riley 2005, p.90
- ↑ Prins 2000, p.143
Masomo zaidi
[hariri | hariri chanzo]- Herbert Prins, Jan Geu Grootenhuis, Thomas T. Dolan (2000). Wildlife Conservation by Sustainable Use. Springer. ISBN 0412797305.
{{cite book}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) - Riley, Laura William (2005). Nature's Strongholds: The World's Great Wildlife Reserves. Princeton University Press. ISBN 0691122199.
- Jolliffe, Lee (2000). Tea and Tourism: Tourists, Traditions and Transformations. Channel View Publications. ISBN 1845410564.
- Nagle, Garrett (1999). Tourism, Leisure and Recreation. Nelson Thornes. ISBN 0174447051.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Lonely Planet Guide Archived 22 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
Serikali ya Wizara na mashirika
- Wizara ya Utalii ya Kenya Archived 6 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- Kenya Tourism Development Corporation Archived 2013-02-18 at Archive.today
- Kenya Wildlife Service Archived 14 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- National Museums of Kenya
- http://www.royaltoursafrica.com/data/attractions/specific/Maasai_Mara_Game_Reserve.vrt Archived 12 Oktoba 2009 at the Wayback Machine.
- http://www.tourism.go.ke/ Archived 6 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- http://en.wikipedia.org/wiki/Tourism_in_Kenya
- https://web.archive.org/web/20061230202343/http://whc.unesco.org/pg.cfm?cid=31&id_site=800
- http://easytravelgear.com
- http://www.ecotourismkenya.org/
- http://www.africaguide.com/country/kenya/accom.htm
- http://www.hmnet.com/africa/kenya/ke_tourist/ke_hotels.html Archived 30 Novemba 2015 at the Wayback Machine.
- http://www.kenyabeach.com/