Shilingi ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shilingi 50
sarafu ya KSh 10

Shilingi ya Kenya (KES au Ksh) ni fedha za Kenya. Shilingi moja imegawanywa kwenye senti mia moja.

Shilingi ya Kenya ilianzishwa mwaka 1966 baada ya kuvunjwa kwa bodi ya fedha ya Afrika ya Mashariki iliyosimamia fedha ya pamoja ya Kenya, Tanzania na Uganda iliyoitwa East African Shilling iliyotumiwa katika maeneo yote yaliyokuwa chini ya Uingereza katika Afrika ya Mashariki.

Kuna sarafu za shilingi 1, 5, 10, 20 na 40.

Sarafu za senti zipo za zamani za senti 1, 5, 10, 20 na 50 lakini hazinunui kitu tena.

Noti zilitolewa za shilingi 5, 10, 20, 50, 100, 200, 500 na 1000 ingawaje noti za shilingi 5, 10 na 20 ni nadra sana kuonekana.

  • Shilingi 1 = Senti 100

Majina ya zamani:

  • Thumuni 1 = Senti 50
  • Peni 1 = Senti 10
  • Ndururu 1 = Senti 5

Sarafu

Benknoti

Benknoti za Kenya 2010
Picha Thamani Ukubwa kwa milimita Rangi Maelezo
Mbele Nyuma Mbele Nyuma Alama
KES0050v.jpg KES0050r.jpg 50 138 × 72 Kahawia-Kijani Picha ya Jomo Kenyatta Sanamu ya ndovu, Mombasa, Ngamia Simba
KES0100v.jpg KES0100r.jpg 100 141 × 74 Dhambarau-Kijani Kenyatta International Conference Centre na sanamu ya Kenyatta, Nairobi
KES0200v.jpg KES0200r.jpg 200 144 × 76 Kijivu-kijani Mavuno ya pamba
KES0500v.jpg KES0500r.jpg 500 147 × 78 Kijivu-kijani Jengo la bunge mjiniNairobi
KES1000v.jpg KES1000r.jpg 1000 150 × 88 Kahawia-kijani Tembo na nyati


ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shilingi ya Kenya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.