Mapinduzi ya kijeshi ya 1982 nchini Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mapinduzi ya kijeshi ya 1982 nchini Kenya ilikuwa jaribio lililoshindikana la kumpindua rais Daniel arap Moi.

Matokeo ya 1982[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 1 Agosti, 1982 , siku ya Jumamosi, kundi la wanajeshi wa anga walivamia kituo cha Redio ya Sauti ya Kenya wakidai kuwa wamepindua Serikali. Kiongozi wao alikuwa Hezekiah Ochuka ambaye pia alikuwa afisa wa ngazi ya chini ya kijeshi akishirikiana na wenzake. Tangazo lao lilisema; "Serikali ya Kenya imepinduliwa na majeshi na sasa iko mikononi mwa majeshi. Viongozi wetu wamekuwa watu wafisadi wenye matumbo makubwa wasiojali maskini."

Tanganzo lilitolewa na kikundi cha wanajeshi waasi lilisababisha watu wengi kuandamana mjini na kupora maduka wakilenga hasa raia wa asili ya Kihindi mjini Nairobi. Inakadiriwa ya kwamba zaidi ya maduka 1,000 yaliporwa na nyumba za Wahindi zilivunjwa na wanawake wao kunajisiwa. Inasemekana kwamba, sababu za kuporwa kwa maduka ya kihindi ilikuwa ni kutokuwepo kwa usawa wa kimaisha kati ya Wakenya na Wahindi mjini Nairobi.

Jeshi la ardhi na polisi walipambana na uasi[hariri | hariri chanzo]

Jaribio la mapinduzi halikudumu kwa muda mrefu baada ya jeshi la ardhi pamoja na polisi kuingia kati na kupambana na uasi kwa baada ya masaa sita tu. Rais Moi alikuwa nje ya Nairobi na mipango ya kurusha mabomu kwa nyumba yake huko Kabarnak haikutekelezwa.

Hezekiah Ochuka alipanda ndege na akakimbilia Tanzania alipokamatwa na kurudishwa Kenya baadaye alipopelekwa mahakamani na kuhukumiwa kunyongwa kama msaliti.

Nini ilikuwa sababu za uasi?[hariri | hariri chanzo]

Idadi kubwa ya viongozi wa uasi walikuwa wanajeshi kutoka kabila la Waluo. Inasemekana kwamba jaribio la mapinduzi lilisababishwa na azimio la Bunge la Kenya la tar. 9 Juni 1982 lililofanya Kenya kuwa nchi ya Chama kimoja. Sheria hii ilizuia jaribio la kiongozi wa Kiluo Jaramogi Oginga Odinga kuanzisha chama cha upinzani.

Nini kilifuata baada ya kushindwa kwa jaribio la Mapinduzi?[hariri | hariri chanzo]

Uasi ulisababisha ukandamizi mkubwa sana. Polisi walipita katika nyumba za askari wa anga pia katika mitaa ya vibanda ambako maelfu ya wakaazi walikamatwa. Pia Jeshi la anga lilifutwa kufuatia tuhuma za kushindwa kutekeleza vema majukumu yake. Jumla ya watu 145 waliuawa ama na waasi au baadaye katika ukandamizi wake.

Viongozi wa Waluo walikamatwa pia; Jaramogi Odinga alifungwa katika nyumba yake na kushtakiwa lakini mashatki yaliondolewa baadaye lakini mwanake Raila Odinga alifungwa jela kwa miaka sita hata bila kuhukumiwa.

Kwa jumla siasa ya rais Moi ilibadilika kuwa ya kidikteta baadaye na polisi ilipewa mamlaka pana kutafuta wapinzani kata kuwatesa na kuwakamata bila kuwapeleka mahakamani.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]