Nembo ya Kenya huonyesha simba wawili wanaoshika mishale na ngao ya Maasai. Ngao huoneyesha rangi za taifa zilizogawanyika katika sehemu nne.
Nyeusi humaanisha watu wazaliwa Kenya
Kijani humaanisha kilimo na maliasili
Nyekundu humaanisha mapambano kupata uhuru
Nyeupe humaanisha umoja na usalama
Sehemu nyekundu huonyesha jogoo anayeshika shoka; hii humaanisha maisha bora.
Ngao na simba wamesimama juu ya Mlima Kenya. Chini ya ngao kimeandikwa Harambee.