Nenda kwa yaliyomo

Mikoa ya Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikoa ya Kenya ilivyokuwa.

Mikoa ya Kenya (kwa Kiingereza "Provinces of Kenya") ilikuwa mgawanyo wa kiutawala kwenye ngazi ya juu nchini Kenya. Taifa liligawanywa katika mikoa minane (tazama ramani). Mikoa hii iligawanywa katika wilaya 46 ambazo ziligawanywa zaidi katika tarafa 262. Tarafa ziligawanywa katika lokesheni 2427, na kisha lokesheni ndogo 6612[1] Kila mkoa ulisimamiwa na Mkuu wa Mkoa (PC).

Serikali za wilaya za Kenya zaidi hazikufuata mipaka yna tarafa. Zimejumuishwa kama Mabaraza ya Majiji, Manispaa, Miji au ya Kaunti.

Aina ya tatu ya mgawanyiko ni sehemu za uwakilishi bungeni au majimbo. Sehemu hizi ziligawanywa zaidi katika kata.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 ilifuta ngazi ya mikoa. Tangu mwaka 2013 wilaya za Kenya ni ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala. Kuna wilaya 47 nchini Kenya ambazo ni maeneo ya kujichagulia bunge na serikali ya kieneo.

  1. Mkoa wa Kati
  2. Mkoa wa Pwani
  3. Mkoa wa Mashariki
  4. Nairobi (Mji Mkuu)
  5. Mkoa wa Kaskazini Mashariki
  6. Mkoa wa Nyanza
  7. Mkoa wa Bonde la Ufa
  8. Mkoa wa Magharibi

Angalia Pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Afisi Kuu ya Takwimu (Kenya): Katografia ya sensa: Tajiriba ya Kenya Archived 3 Machi 2016 at the Wayback Machine.