Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya)
| ||
Makao Makuu | Garissa | |
’‘‘Mji Mkubwa’’’ | Garissa | |
Eneo - Jumla |
Nafasi ya 3 kati ya mikoa ya Kenya 126,186 km² | |
Wakazi (kadirio) - Jumla (2007) - Msongamano wa watu / km² |
Nafasi ya 8 kati ya mikoa ya Kenya 459,000 4 /km² | |
Lugha mkoani | Kisomali Kioromo | |
Kaskazini-Mashariki ulikuwa mmoja kati ya mikoa 9 ya Kenya. Eneo lake lilikuwa km² 127 000 [1] Ilihifadhiwa 29 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine. na wakazi 962,143 (sensa ya 1999).
Wakati wa ukoloni eneo hilo liliitwa "Northern Frontier District" (Eneo la mpakani wa kaskazini) likitawaliwa pekee na sehemu kubwa ya Kenya.
Wakazi walio wengi ni Wasomalia kwa lugha na utamaduni; kuwepo kwao ndani ya Kenya badala ya Somalia ni urithi wa mipaka ya kikoloni. Wengine ni Waborana, Warendille na Waturkana.
Kuna pia makambi makubwa ya wakimbizi Wasomalia, hasa karibu na Daadab.
Hali ya hewa
[hariri | hariri chanzo]Eneo hili ni kavu sana. Mbali na bonde la mto Tana na maeneo mengine madogo, mkoa haufai kwa kilimo. Wakazi walio wengi hujipatia riziki kutokana na ufugaji.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Mkoa wa Kaskazini-Mashariki ulikuwa na wilaya nne:
- Garissa -- makao makuu Garissa
- Ijara -- makao makuu Ijara
- Wajir -- makao makuu Wajir
- Mandera -- makao makuu Mandera
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Kaskazini-Mashariki (Kenya) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |