Waborana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Waborana
Boranamanvoting4.JPG
Mtu mwenye asili ya Kiborana akipiga kura katika kituo cha upigaji kura Marsabit, Kenya.
Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana
Ethiopia, Kenya
Borana pia ni jina la Kihispania la kundi la Boran, ambalo linajumuisha tabaka kubwa la lugha la Witotoan.

Bobana Oromo ambao pia huitwa Boran ni jamii ipatikanayo Kusini mwa Ethiopia, Oromai na Kaskazini mwa Kenya[1] ambao wanajulikana kuwa wafugaji. Wao ni Kundi dogo la Oromo[2]. Wanawakilisha nusu ya makundi mawili ya Waoromo wa Kiasili, nusu nyingine ikiwa Barentu.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Waoromo wa Kaskazini mwa Kenya waliingia eneo hilo mara ya Kwanza kutoka Kusini mwa Ethiopia wakati wa uhamizi mkubwa wa Karne ya Kumi. Walitawanyika kuwa Waborana wafuga Ng'ombe na wafuga Ngamia, Wagabra na Wasakuye[3].

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Waborana huzungumza Kiborana (au afaani Boraana), ambayo ni mojawapo ya sehemu ya Kushaiti (Cushite) ambayo pia ni mojawapo ya kundi kubwa la Afro-Asiatic. Takribani watu milioni 7 wanajitambulisha na jamii ya Borana.

.

Kalenda ya Kiborana[hariri | hariri chanzo]

Inaaminika kuwa Waborana wana Kalenda yao waliyoitunga karibu miaka ya 300 BC. Kalenda yao ni mfumo wa lunar-stellar, ambayo hutegemea matukio ya anga ya mwezi pamoja na Nyota Saba. Miezi ya Kiborana (Mizunguko ya miezi na nyota) ni: Bittottessa (iangulum), Camsa (Pleiades), Bufa (Aldebarran), Waxabajjii (Belletrix), Obora Gudda (Orion-Saiph ikiwa kati), Obora Dikka (Sirius), Birra (Mwezi mzima), Cikawa (gibbous moon), Sadasaa (Nusu-mwezi), Abrasa (Kipande kikubwa cha mwezi), Ammaji (Kipande cha wastani), na Gurrandala (Kipande kidogo)[4].

Matabaka madogo[hariri | hariri chanzo]

Waoromo wanjumuisha makundi mawili muhimu, ambayo hugawanyika katika koo nyingi za kifamilia. Kutoka Magharibi kuelekea Mashariki na Kaskazini kuelekea Kusini, matabaka hayo ni:

...Na vijikundi vingi vingine

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Vidokezo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ethnologue;Ethnologue
  2. Aguilar, Mario. The Eagle as Messenger, Pilgrim and Voice: Divinatory Processes among the Waso Boorana of Kenya. Journal of Religion in Africa, Vol. 26, Fasc. 1 (Feb., 1996), pp. 56-72. Iliwekwa mnamo 2007-10-27.
  3. Elliot M. Fratkin, Eric Abella Roth, As Pastoralists Settle, (Springer: 2005), p.39
  4. Lawrence R. Doyle, The Borana Calendar REINTERPRETED

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

Kusoma zaidi[hariri | hariri chanzo]

  • Asmerom Legesse, Gada
  • Beckingham and G.W.B. Huntingford, Some records of Ethiopia Hakluyt Society, 1954
  • Bassi Marco, Decisions in the Shade. Political and juridical processes among the Oromo-Borana Red Sea Press, 2005