Homa ya manjano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
njano jack
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10A95.
ICD-9060
DiseasesDB14203
MedlinePlus001365
eMedicinemed/2432 emerg/645
MeSHD015004

Homa ya manjano (pia: Homanyongo, inayojulikana kwa Kiingereza kama yellow jack au yellow plague,[1]) ni ugonjwa mkali unaosababishwa na virusi.[2]

Katika kesi nyingi, dalili hujumuisha homa, homa ya baridi, kukosa hamu ya chakula, kichefuchefu, maumivu ya misuli hasa mgongoni, na maumivu ya kichwa.[2] Kwa kawaida dalili hupona kwa siku tano.[2]

Kwa watu wengine baada ya kupata nafuu, homa hurudi, maumivu ya fumbatio hutokea, na uharibifu wa ini huanza na kusababisha ngozi ya njano.[2] Ikiwa hii itatokea, hatari ya kuvuja damu na matatizo ya figo unaongezeka.[2]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Ugonjwa huu unasababishwa na virusi vya homa ya manjano na kusambazwa kwa kuumwa na mbu wa kike.[2] Vinaambukiza tu binadamu, mamalia wa hali ya juu na spishi nyingi za mbu.[2] Katika miji, husambazwa kwa kawaida na mbu wa spishi wa Aedesaegypti.[2]

Virusi ni Virusi vya RNA vya jenasi Flavivirus.[3] Ugonjwa huu unaweza kuwa ngumu kueleza lakini maradhi mengine tu, hasa katika awamu za kwanza.[2] Ili kuthibitisha hali hiyo, uchunguzi wa sampuli ya damu wa polymerase chain reaction unahitajika.[4]

Kinga, tiba na matarajio[hariri | hariri chanzo]

Chanjo bora na salama dhidi ya homa ya manjano ipo, na baadhi ya nchi hudai chanjo ya wanaosafiri.[2] Juhudi nyingine za kuzuia maambukizi zinajumuisha upunguzaji wa idadi ya mbu wanaosambaza virusi.[2]

Katika maeneo ambayo homa ya manjano ni ya kawaida na hakuna chanjo, utambuzi wa mapema wa ugonjwa na uchanjaji wa sehemu kubwa ya idadi ya watu ni muhimu ili kuzuia mlipuko.[2]

Ukiwa umeambukizwa, udhibiti ni wa dalili na hakuna hatua maalum dhidi ya virusi haswa.[2] Kwa wale walio na ugonjwa mkali, kifo hutokea kwa takriban nusu ya watu wasiokuwa na matibabu.[2]

Uenezi na historia[hariri | hariri chanzo]

Homa ya manjano husababisha maambukizi 200,000 na vifo 30,000 kila mwaka,[2] takriban asilimia 90 ya hayo yakitokea barani Afrika.[4]

Karibu bilioni moja ya watu wanaishi katika eneo la dunia mahali ugonjwa huo ni wa kawaida.[2] Inapatikana sana katika maeneo ya tropiki Amerika Kusini na Afrika, lakini si Asia.[5][2]

Tangu miaka ya 1980, idadi ya kesi za homa ya manjano zimekuwa zikiongezeka.[6][2] Hii inaaminika ni kwa sababu watu wachache wana kingamwili, watu wengi wakiishi kwa miji, na watu wanaosafiri kila mara, na mabadiliko ya hali ya hewa.[2]

Ugonjwa ulianzia barani Afrika, ambapo ulisambaa Amerika Kusini kupitia biashara ya utumwa katika karne ya 17.[1] Tangu karne ya 17 milipuko ya ugonjwa umetokea Marekani, Afrika na Uropa.[1] Katika karne za 18 na 19, homa ya manjano ilionekana kama ugonjwa wa kuambukiza hatari sana.[1] Virusi vya homa ya manjano vilikuwa virusi vya kwanza vya binadamu kugunduliwa.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Oldstone, Michael (2009). Viruses, Plagues, and History: Past, Present and Future. Oxford University Press. ku. 102–4. ISBN 9780199758494. 
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 2.15 2.16 2.17 2.18 "Yellow fever Fact sheet N°100". World Health Organization. May 2013. Iliwekwa mnamo 23 February 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. 3.0 3.1 Lindenbach, B. D., et al. (2007). "Flaviviridae: Virusi na marudio yake". Katika Knipe, D. M. and P. M. Howley. (eds.). Fields Virology (toleo la 5th). Philadelphia, PA: Lippincott Williams &Wilkins. uk. 1101. ISBN 0-7817606-0-7. 
  4. 4.0 4.1 Tolle MA (April 2009). "Mosquito-borne diseases". CurrProblPediatrAdolesc Health Care 39 (4): 97–140. PMID 19327647. doi:10.1016/j.cppeds.2009.01.001.  Check date values in: |date= (help)
  5. "CDC Yellow Fever". Iliwekwa mnamo 2012-12-12. 
  6. Barrett AD, Higgs S (2007). "Yellow fever: a disease that has yet to be conquered". Annu. Rev. Entomol. 52: 209–29. PMID 16913829. doi:10.1146/annurev.ento.52.110405.091454.