Nenda kwa yaliyomo

Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la mbuga kando la Ziwa Nakuru
Ndege za Heroe ziwani

Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru ni mbuga ya wanyama nchini Kenya iliyoko kando ya Ziwa Nakuru, karibu na mji wa Nakuru. Umbali wa Nairobi ni km 140. Geti kuu liko kilomita 4 kutoka mji wa Nakuru. Eneo lake ni takriban km² 188. Inajulikana hasa kwa wingi wa ndege aina ya heroe na kundi la vifaru ambao wanaonekana hapa kwa uhakika mkubwa kulingana na mbuga nyingine za Kenya.

Mbuga ilianzishwa mwaka 1961. Sababu ya kuianzisha ilikuwa idadi kubwa ya ndege wa heroe wanaokusanyika hapa. Wakati mwingine huhesabiwa kuwa hadi milioni mbili. Idadi ya heroe hubadilika kimajira kulingana na kiasi cha algae ambazo ni chakula chao hasa.

Baadaye vifaru walipelekwa hapa wakati walivindwa ovyo katika mbuga nyingine nchini na kuwa hatarini mwa kupotea. Leo hii kuna takriban vifaru 60 mbugani wanaolindwa na walinzi wa pori. Hadi leo watoto yatima wa vifaru wanaopatikana katika mbuga mbalimbali wanapelekwa hapa. Vilevile kama hali ya uwindaji ovyo unazidi katika eneo fulani na walinzi walishindwa kuukomesha vifaru walitiwa sindano ya kuwatuliza, kukamatwa na kupelekwa Nakuru. Kutokana na hali ya kuhatarishwa kwa vifaru mbuga yote imezungukwa na fensi.

Nje ya vifaru kuna takriban spishi 56 za mamalia mbalimbali pamoja na spishi 450 za ndege.


Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]