Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya mlima wa pili kwa urefu barani Afrika, Mlima Kenya. Picha iliyopigwa na Håkon Dahlmo mnamo agosti 2003.

Mbuga ya Taifa ya Mlima Kenya 0°07′26″S 37°20′12″E / 0.12389°S 37.33667°E / -0.12389; 37.33667, iliyoanzisha mwaka wa 1949, hulinda kanda inayozunguka Mlima Kenya. Awali ilikuwa ni hifadhi ya misitu kabla ya kutangazwa kama mbuga ya kitaifa. Hivi sasa ni mbuga ya taifa ndani ya hifadhi ya misitu ambayo imeizunguka.[1]Mnamo Aprili mwaka wa 1978 eneo hilo lilifanywa hifadhi ya Biosphere ya UNESCO. [2] Mbuga ya taifa na hifadhi ya misitu ziliunganishwa zikawa katika orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO mwaka wa 1997.[3]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Kenya Wildlife Service (2007). "Mount Kenya National Park". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-22. Iliwekwa mnamo 2008-02-23. 
  2. United Nations Environment Programme (1998). "Protected Areas and World Heritage". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-12. Iliwekwa mnamo 2008-02-23. 
  3. United Nations (2008). "Mount Kenya National Park/Natural Forest". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-12-30. Iliwekwa mnamo 2008-02-23.