Hifadhi ya Taifa ya Amboseli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Hifadhi ya Taifa ya Amboseli, ambayo zamani ilikuwa inaitwa hifadhi ya wanyama ya Maasai Amboseli, iko katika Wilaya ya Kajiado, Mkoa wa Bonde la Ufa, nchini Kenya. Mbuga hii ina ukubwa wa eneo wa kilomita 390 katika msingi wa eneo la kilomita 8,000 na inaenea mpakani mwa Kenya na Tanzania. Jina "Amboseli" linatokana na lugha ya Kimasai ikimaanisha vumbi lenye ladha ya chumvi.

Wenyeji wa sehemu hii ni Wamasai, lakini watu kutoka maeneo mengine ya nchi wanakaa huko kwani walivutiwa na uchumi uliofanikiwa na ambao ulisababishwa na utalii na kilimo kabambe kandokando ya mifumo ya mabwawa ambayo yanaifanya eneo hili lenye mvua kidogo (wastani wa milimita 350 kwa mwaka) kuwa mojawapo ya sehemu bora duniani kuwatazama wanyamapori. Mbuga hii hulinda mabwawa mawili kwa matano ambayo yako, na inahusisha ziwa lililokauka la Pleistocene na mimea yenye nusu-ukame.

Viungo vya njə[hariri | hariri chanzo]