Nenda kwa yaliyomo

Utalii nchini Lesotho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utalii nchini Lesotho ni sekta inayokua kwa kasi nchini humo.

Mwaka 2013 utalii huo umechangia takribani asilimia 5.5 kwenye pato la nchi ya Lesotho na inategemea kuongezeka mpaka asilimia 6.1 ifikapo mwaka 2024. Sekta hiyo imeajiri jumla ya watu 25,000 mwaka 2013 ambayo ni asilimia 4.6 ya ajira nchini humo.

Makazi ya Afrika kusini yanayoizunguka Lesotho yanaunda jumla ya asilimia 90 ya wageni nchini humo. Safari nyingi ni kwaajili ya kutembelea ndugu na marafiki.

Harakati mbalimbali za nje ndio zinaunda shughuli mbalimbali za burudani kwaajili ya watalii nchini humo. Sehemu za milima zinavutia utalii WA kupanda, utalii wa farasi na mchezo wa kuteleza kwenye theluji pamoja na kutumia kutumia magari yenye uwezo WA kutalii njia mbalimbali. Hotel ya Afriski ski hufanya kazi kipindi cha baridi.

Njia zinazotumika sana kuingilia nchini Lesotho ni uwanja wa ndege wa Moshoeshoe na mipaka ya Maseru na Maputsoe.[1]

Utalii nchini humo unasimamiwa na wizara ya utalii, mazingira na utamaduni iliyopo mji mkuu Maseru.