Maseru
Mandhari
Jiji la Maseru | |
Nchi | Lesotho |
---|


Maseru ni mji mkuu wa Lesotho na mji mkubwa ukiwa na wakazi 330,760 (2016). Maseru iko kwa mto Caledon (Mohokare). Chuo Kikuu cha Lesotho na kiwanja cha kimataifa cha ndege ni karibu na mji.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ilikuwa kituo kidogo cha biashara ilipoteuliwa na chifu Moshoeshoe I wa Wasotho kuwa mji mkuu wake mwaka 1869.
Tangu mwaka 1884 hadi 1966 ilikuwa mji mkuu wa nchi lindwa ya "Basutoland" chini ya Uingereza. Mwaka 1966 ikawa mji mkuu wa Lesotho huru.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Kuna viwanda vya kutengenezea mishumaa na matandiko ya zulia. Kuna pia viwanda vya vitambaa kwa ajili ya soko la Marekani.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Maseru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |