Soko la Hisa la Nairobi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Soko la Hisa la Nairobi (NSE) ndilo soko kuu la kuuza na kununua Hisa nchini Kenya. Lilianza mwaka wa 1954 kama Soko la Hisa la Ng'ambo wakati Kenya ilikuwa bado chini ya Ukoloni wa Uingereza kwa ruhusa ya Soko la Hisa la London. NSE ni mwanachama wa Shirikisho la Masoko ya Hisa ya Afrika.

Soko la Hisa la Nairobi ndilo la nne kwa ukubwa Afrika katika mtazamo wa idadi ya hisa zinazouzwa, na la tano katika Thamani ya Hisa zote kama asilimia ya Pato la Taifa.[1] Soko hili hufanya kazi kwa ushirikiano na Soko la Hisa la Uganda na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam, pamoja na kusajili hisa mbalimbali katika masoko yote matatu.

Soko hili lina vikao vya kabla kati ya 09:00-09:30 na vikao vya biashara ya kawaida kati ya 09:30-03:00 siku zote za wiki isipokuwa Jumamosi, Jumapili na sikukuu zinazotangazwa na Soko mapema.[2]

Ofisi na sakafu ya biashara za NSE ziko katika jumba la Nation Centre katika baraste ya Kimathi. Biashara hufanywa kupitia Electronic Trading System (ETS) ambayo ilikamilika mwaka wa 2006. Mtandao wa Wide Area Network (WAN) uliwekwa mwaka wa 2007 na hili lilitupilia mbali haja ya Kampuni za kuuza na kununlia Hisa kuwapeleka mawakala wao (wafanyabiashara) kwenye ukumbi wa biashara ili kuuza au kununua hisa. Kwa sasa, shughuli za kununua na kuuza hufanywa kutoka ofisi zao kupitia mtandao wa WAN. Hata hivyo, baadhi ya mawakala bado wanaweza kufanya biashara kutoka sakafu ya NSE.

Fahirisi mbili hutumiwa kwa kawaida kupima utendaji. Ile ya NSE 20-Share Index imetumiwa tangu mwaka wa 1964 na hupima utendaji wa kampuni 20 bora zilizo na msimamo mzuri kifedha na ambazo zimezidi kurejesha matokeo mazuri ya kifedha mfululizo. Zilizojumuishwa katika fahirisi hii ni Kampuni ya Sukari ya Mumias, Express Kenya, Rea Vipingo, Sasini Tea, CMC Holdings, Kenya Airways, Safaricom, Nation Media Group, Barclays Bank Kenya, Equity Bank, Kenya Commercial Bank, Standard Chartered Bank, Bamburi Cement, British American Tobacco, Kengen, Centum Investment Company, East African Breweries, EA Cables, Kenya Power & Lighting Company Ltd na Athi River Mining. Fahirisi hii haswa hulenga mabadiliko ya bei ya makampuni haya 20.

Mwaka wa 2008, NSE All Share Index (NASI) ilianzishwa kama fahirisi mbadala. Kipimo chake ni kiashiria cha utendaji wa soko kwa jumla. Fahirisi hii hujumuisha hisa zote zilizouzwa au kununuliwa kila siku. Hivyo basi mtazamo wake ni utendaji kwa ujumla wa thamani ya hisa zote katika soko badala ya mabadiliko ya bei ya Hisa chache teule.

Hata hivyo kuna fahirisi nyingine ya tatu; AIG 27 Index ambayo hulinganishwa mabadiliko ya bei ya hisa za makampuni 27 ambazo zimetambuliwa kama zilizo imara kiasi. Wazo la msingi la fahirisi hii inalingana na ile ya NSE 20-Share Index. Lakini ilhali ile ya AIG imebainishwa na kampuni ya AIG (kampuni ya huduma za kifedha na sehemu ya AIG Group), ile ya NSE 20-share Index ni ya Soko la Hisa la Nairobi.

Kampuni zilizosajilishwa[hariri | hariri chanzo]

Kampuni zilizokuwa zimesajilishwa kufikia Aprili 2008:

Soko kuu[hariri | hariri chanzo]

(MIMS)

Sekta ya kilimo[hariri | hariri chanzo]

Kifupisho Kampuni Vidokezo
-- Kakuzi Kahawa, chai, matunda ya passion, avocado, machungwa, mananasi, zingine
RVP Rea Vipingo Sisal Estate Katani
STC Sasini Tea and Coffee chai, kahawa
-- Unilever Tea --

Biashara na Huduma[hariri | hariri chanzo]

Kifupisho Kampuni Vidokezo
-- Access Kenya Group mtoa huduma tovuti
-- Car General Kenya --
CMC CMC Holdings Cooper Motor Corporation; usambazaji wa magari
HBL Hutchings Biemer Limited samani
KAL Kenya Airways Shirika la Safari za ndege la Kenya; limesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda na Dar es Salaam
-- Marshalls EA magari
NMG Nation Media Group magazeti, majarida,stesheni za redio na televisheni
-- Safaricom Simu ya mkononi
-- Scangroup Kenya matangazo na mauzo
-- Standard Group Ltd mchapishaji gazeti
TPS TPS Serena Huduma ya kuchangia Utalii; Hoteli na Maeneo ya Starehe
USL maduka ya Uchumi --

Viwanda[hariri | hariri chanzo]

Kifupisho Kampuni Vidokezo
ARM Athi River Mining saruji, mbolea, madini; kuchimba migodi na uundaji
BCC Bamburi Cement saruji
BOC BOC Kenya Oksijeni ya Afrika Mashariki
BAT British American Tobacco Limited --
-- British Oxygen Kenya oksijeni
CIL Carbacid Investments dioksidi kaboni
CBL Crown-Berger (Kenya) rangi
ECL EA Cables utengenezaji wa nyaya
EPC EA Portland Cement saruji ya Portland
-- East African Breweries bia; imesajiliwa katika masoko ya Hisa ya Uganda na Dar es Salaam
-- EVEREADY East Africa betri, vinyozi vya kutumia na kutupa
-- Kengen uzalishaji umeme
KOC Kenya Oil mafuta ya petroli
MSC Kampuni ya Sukari ya Mumias mashamba na utengenezaji wa sukari
-- Olympia Capital Holdings vigae vya sakafu vya vinyl; mabati ya vinyl; vigae vya mpira; vifaa vya ujenzi
-- Sameer Group Teknolojia, Biashara ya kilimo, viwanda, usafiri
TKL Total Kenya mafuta ya petroli
UGL Unga Group kusaga unga

Fedha na Uwekezaji[hariri | hariri chanzo]

Kifupisho Kampuni Vidokezo
BAR Barclays Bank of Kenya --
-- Centum Investment Company --
CFC CFC Stanbic Bank benki, uwekezaji
DTB Diamond Trust Bank of Kenya benki, uwekezaji
EBL Equity Bank Group imesajiliwa pia katika Soko la Hisa la Uganda
HFC Housing Finance Company mortgage
JIC Jubilee Insurance imesajiliwa pia katika Soko la Hisa la Uganda
KCB Kenya Commercial Bank benki & uwekezaji. imesajiliwa pia katika masoko ya Hisa ya Uganda, Dar es salaam na Rwanda
-- Kenya Re-Insurance Corporation bima
NBK National Bank of Kenya --
NIC National Industrial Credit Bank --
PAI Pan Africa Insurance --
SCB Benki ya Standard Chartered --

Soko la uwekezaji mbadala[hariri | hariri chanzo]

(AIMS)

Kifupisho Kampuni Vidokezo
ABC A Baumann mashine
CTL Citytrust Ltd huduma za kifedha
EAL Eaagads Kahawa
Exp Express Kenya logistiki
KTC Kapchorua Tea --
-- Kenya Orchards matunda, hifadhi, juisi
LTC Limuru Tea --
GWK Williamson Tea Kenya --

Soko la Mapato yasiyobadilika[hariri | hariri chanzo]

(FISMS)

Kifupisho Kampuni Vidokezo
-- Kenya Power Lighting Ltd 7% PREF usambazaji umeme, usambazaji na reja
-- Kenya Power Lighting Ltd 4% Preferred --

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Flag-map of Kenya.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Soko la Hisa la Nairobi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.