Crown Berger (Kenya)
Crown-Berger (Kenya) ni kampuni ya rangi nchini Kenya; iliyoanzishwa mwaka wa 1958 na hushiriki katika utengenezaji na usambazaji wa rangi. Crown-Berger ina makao yake makuu mjini Nairobi imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi.
Bidhaa
[hariri | hariri chanzo]Bidhaa za kampuni hii zinahusu:
- rangi ya viwanda
- rangi ya marina
- rangi ya magari
- rangi ya mbao na kadhalika.
Kampuni hii inahusika na kununua na kusafirisha rangi kutoka ng'ambo. Inanunua kutoka kampuni maarufu kama PPG ya Ufaransa, Ferro ya Afrika Kusini,Asian Paints na Berger Internationa ya Dubai na Singapore.Iliendelea katika mpango wke wa upanuzi na kuanzisha bidhaa kaika jina ya "Regal Brand" nchini Uganda. Crown-Berger (Kenya) ina zaidi ya wauzaji wadogo na wakubwa 1500 katika mfumo wao wa usambazaji.
Kampuni hii inaendesha vituo Nairobi,Mombasa,Kisumu na Kampala na ,hivi sasa, ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 1 kila mwezi.
Sehemu ya 'wajibu wa kampuni' ya tovuti ya Crown-Berger (Kenya) inaonyesha msaada wa kampuni katika kuandaa michezo na miradi ya kupodoa miji.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Crown-Berger Kenya Ilihifadhiwa 16 Desemba 2009 kwenye Wayback Machine.