Nation Media Group

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nation Center.jpg

Nation Media Group (NMG) ni kundi la vyombo vya habari vya Kenya lililoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi.[1] NMG ilianzishwa na Aga Khan IV mwaka wa 1959 na ndilo shirika kubwa la binafsi la vyombo vya habari katika Afrika Mashariki na Kati na lina maofisi nchini Kenya, Uganda na Tanzania.[2] Mwaka wa 1999, NMG ilianzisha NTV, kituo cha habari nchini Uganda, na Easy FM.[3]

Tangu 2001 NMG imemiliki kampuni ya habari ya Tanzania ianayoitwa Mwananchi Communications Ltd. yenye kutoa magazeti kama vile Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen.

Katika Kenya na Uganda NMG inachapisha The EastAfrican, Daily Nation (gazeti kuu nchini Kenya), The Business Daily, Daily Monitor, NMG Investor Briefing , Taifa Leo na Zuqka.

  1. http://stockskenya.com/newsite/stkprofiler.aspx?stkId=10
  2. http://www.nation.co.ke/meta/-/1194/1172/-/ojmv8c/-/index.html
  3. http://www.nation.co.ke/meta/-/1194/1172/-/ojmv8c/-/index.html

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]