Soko la Hisa la Uganda
Mandhari
Soko la Hisa la Uganda ni soko la hisa la pekee nchini Uganda. Makao makuu yapo Kampala. Likaanzishwa mwaka 1197 na kuanza shughuli kwenye Januari 1998. Kazi yake inasimamiwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji ya Uganda (Uganda Capital Markets Authority) iliyoko chini ya Benki Kuu ya Uganda. Ni mwanachama wa ushirikiano wa masoko ya hisa ya Afrika.
1998 hisa za pekee zilizofanyiwa biashara zilikuwa zile za Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) na hadi sasa kuna makampuni 9 katika Afrika ya Mashariki yaliyoandikishwa sokoni. Siku za biashara ni Jumatatu, Jumanne na Alhamisi.
Makampuni
[hariri | hariri chanzo]- Uganda Clays
- British American Tobacco Uganda/British American Tobacco/BATU - tumbako
- Bank of Baroda Uganda/Bank of Baroda - benki
- DFCU Group - benki
- New Vision Printing and Publishing Company - uchapaji
- Jubilee Holdings Limited/JHL -
- Kenya Airways
- East African Breweries/EABL - bia
- Stanbic Bank - benki
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiingereza) Soko la hisa la Uganda Archived 4 Machi 2008 at the Wayback Machine.
- (kiingereza) Faida za soko la hisa la Uganda 6 Agosti 2011.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Soko la Hisa la Uganda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |