Nenda kwa yaliyomo

Safaricom

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Safaricom
Makao MakuuKenya Nairobi, Kenya
Mapato kabla ya riba na kodi£131 million (2007)
Net income£88 million (2007)
Tovutiwww.safaricom.co.ke

Safaricom, ni kampuni ya mtandao inayoongoza nchini Kenya. Ilianzishwa mwaka wa 1997 kama raslimali ya Telkom Kenya. Mwezi Mei mwaka wa 2000, kundi la Vodafone PIC kutoka Uingereza, ambalo ndilo kampuni kubwa la mawasiliano duniani, lilimiliki asilimia 40 ya kampuni na usimamizi wa majukumu ya kampuni.

Kuanzia tarehe 17 Mei 2006, Michael Joseph aliteuliwa kuwa afisa mkuu wa kampuni hii. Ripoti za karibuni katika vyombo vya habari zinaonyesha kuwa Vodafone PIC kutoka Uingereza inamiliki asilimia 35 peke yake na asilimia 5 iliyobaki inamilikiwa na kampuni ndogo inayojulikana kama, Mobitelea Ventures Limited, Taarifa hizi zilisabisha mayowe ambapo ilibidi afisa mkuu, Michael Joseph kuitwa mbele ya PIC "Public Investment Committee", ambapo aliweza kukanusha kuwa anajua mbia huyo mwingine. Inaaminika sana kwamba serikali ya zamani iliweza kuashiria Vodafone kuwapa asilimia 5 kama malipo ya kuwapa maafisa wao vyeo vya juu katika utawala. Fursa ya Safaricom kuwapa umma hisa, katika soko la hisa la Nairobi, ilifungwa katikati mwa mwezi Aprili mwaka wa 2008.

Safaricom inaajiri watu zaidi ya 1500 hasa katika vituo vyake katika Nairobi na miji mingine mikubwa kama Mombasa, Kisumu, Nakuru na Eldoret ambayo inasimamia maduka yake. Hivi sasa, iko kila pahali katika taifa hili ili kuhakikisha wateja nchini kote wamepata bidhaa na huduma za kampuni hii.

Kwanzia mwezi wa Oktoba mwaka wa 2007, Safaricom inajivunia kuwa na wigo wa wateja takriban milioni 8, ambao wengi wao wako katika miji mikubwa - Nairobi, Mombasa, Kisumu na Nakuru. Makao makuu ya Safaricom iko katika jumba la Safaricom ,barabara kuu ya Waiyaki katika jiji la Westlands, mjini Nairobi. Ina ofisi nyingine katikati mwa mjini Nairobi katika jengo la I & M, Kenyatta Avenue, mtaa wa Kimathi na kaitka jumba Shankardass ambayo iko karibu na jumba la sinema lijikanavyo kama "Kenya Cinema" mtaani wa "Moi Avenue". mshinani mkuu wa Safaricom ni kampuni ya Kenya ya Zain.

Safaricom huwa na vitendo vya hisani mbapo husaidia jamii ambazo haziwezi kujisaidi kupitia chini katika jamii hasa Safaricom Foundation.

Mnamo Januari 2023, Safaricom ilimleta Adil Khawaja kwenye nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.[1].

Huduma ya Flashback

[hariri | hariri chanzo]

kutokana ugumu wa mapato kwa wateja wengi wa Safaricom, msongamano wa mtandao unasababishwa mbinu inayojulikana kama 'flashing'. "Flashing" ni zoezi la kumpigia mtumiaji simu mwigine , lakini unakata kabla hajajibu baada ya kushikamana. Safaricom imeweza kuotoa huduma ambayo watumiaji wa simu wanaweza kwaarifu wenzao kuwa wangetaka kupigiwa simu kwani hawataweza kulipia. Gharama ya huduma hii ilikuwa bure kwa watumiaji, lakini gharama kubwa katika mtandao .

Hii ndiyo sababu ya safaricom kutoa huduma ya 'Flashback' ambapo ilimpa kila mteja fursa wa kutuma ujumbe mfupi mara tano kwa siku ambapo kila ujumbe una maneno yafuatayo. "Please call me. Thank you ". Ingawa ujumbe unaweza udhi ukitumwa kwa nia isiyo na maana ni muhimu sana wakati mmoja ambapo mtumiaji wa simu yupo taabuni na hana pesa kwa simu yake. Hii pia inaweza kuwa sababu ya wazazi kuwanunulia watoto wao bila kujali kuweka pesa katika simu hizi. Bahati mbaya ni kuwa , huduma hii inatumika katika mtandao wa safaricom peke yake kutokana na ugumu wa uwelewano na Zain, mshindani mkuu wa safaricom.

Huduma za pesa kupitia ujuzi wa umeme

[hariri | hariri chanzo]

Safaricom wameweza kuleta maendeleo taifa lote kwa kuanzisha huduma za ya benki kupitia simu iitwayo M-Pesa, ambayo inawaruhusu wakenya kutuma na kupokea pesa kutmia njia ya ujumbe mfupi. [1] Huduma hii haihitaji mtu kuwa na akaunti ya benki, ni jambo la muhimu sana katika nchi kama Kenya, ambapo watu wengi hawana akaunti ya benki. Kutumia M-Pesa, mtumiaji anaweza kununua pesa saa yoyote katika kituo cha M-Pesa na kutuma kupitia katika hali ya umeme katika mtumiaji simu mwingine yeyote nchini Kenya,ambaye anaweza kubadilisha kuwa pesa halali katika kituo chochote cha M-Pesa. Mfumo huu unaweza kulinganishwa na hawala au huduma zaWestern Union. Simu ambayo inahuduma za M-Pesa inaweza linganishwa nawaletiambayo unaweza shilikia hadi shilingi 50,000 za Kenya.[2] Wadau wa Safaricom Vodafone, ambayo ilishiriki katika uanzishaji wa M-Pesa, ilitangaza kwamba inakusudia kuenza M-Pesa kuwa huduma ya kimataifa .

Huduma nyingine

[hariri | hariri chanzo]

Safaricom pamoja na makampuni mengine mengi wameanzisha huduma mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya umma kuanzia hali ya anga , bei ya soko na hata burudani .

  1. http://news.bbc.co.uk/1/hi/technology/6241603.stm
    http://www.safaricom.co.ke/m-pesa/ Archived 8 Machi 2007 at the Wayback Machine.
    http://www.economist.com/printedition/displayStory.cfm?story_id=9414419
  2. "Safaricom m-pesa - FAQs". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-02. Iliwekwa mnamo 2009-12-08.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]