Nenda kwa yaliyomo

Westlands (Nairobi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Westlands)
Waiyaki Way karibu na Kangemi, Westlands Nairobi
Westlands

Westlands ni mtaa wa jiji la Nairobi (Kenya) ulioendelea kuwa kitovu cha biashara kando ya Nairobi mjini. Westlands iko kando ya barabara kuu ya Waiyaki Way na kipilefti ya Westlands. Ni pia jina la moja kati ya tarafa nane za Kaunti ya Nairobi.

Hadi miaka ya 1980 Westlands ilikuwa sehemu tulivu ya nyumba za watu na maduka machache ikahesabiwa kuwa sehemu ya Parklands. Katika nusu ya pili ya miaka ya 1980 majengo makubwa ya maduka kama "The Mall" na baadaye "Sarit Center" yalijengwa yaliofuatwa na nyumba za ofisi. Wenye biashara na ofisi wamependa Westlands kwa sababu inafikiwa kwa urahisi kutoka pande za kaskazini na magharibi za Nairobi bila kuingia katika msongamano wa magari mjini penyewe; pia kwa sababu hali ya usalama barabarani ni afadhali.

Tarafa ya Westlands

[hariri | hariri chanzo]

Westlands ni pia jina la tarafa inayounganisha maeneo yenye nyumba nzuri kama vile Lavington au Highridge lakini pia mitaa ya vibanda kama Kangemi.

Pamoja na kitovu cha biashara karibu na kipilefti ya Westlands kuna divisheni zifuatazo: