Mto Nairobi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mto Nairobi

Mto Nairobi ni mto unaopitia Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Ndio mto mkuu katika beseni ya mito ya Nairobi, mtandao wa mito kadhaa inayopita sambamba kuelekea mashariki. Mito yote katika beseni hiyo hukutana katika mashariki ya Nairobi na kuungana na Mto Athi, hatimaye kuelekea Bahari ya Hindi. Mingi ya mito hii ni miembamba na michafu sana. Mkondo kuu, Mto Nairobi, umeweka mpaka wa kaskazini mwa jiji. Mto huu umefanywa kanali katika sehemu zingine.

Mto Nairobi una vijito kadhaa, kama vile (katika utaratibu wa kushuka kutoka kaskazini hadi kusini):

Mto Motoine unafululiza katika Dimbwi la Nairobi, ziwa lililofanywa na wanadamu kutoa maji ya kunywa kwa wakazi wa Nairobi. Mbele zaidi huendelea kama Mto Ngong.

Mito ya Nairobi huchafuliwa na taka kutoka kilimo, makazi duni na viwanda[1] Baadhi ya kingo za mito pia zinajulikana kwa sifa mbaya ya ukosefu wa usalama. Mito hii hugawanya mji kutokana na ukosefu wa mapito yafaayo.

Wakati wa misimu ya mvua maji huongezeka, na kusababisha athari ya mafuriko katika mito yenye kingo zilizo chini.

Kuna mto wa pili uitwao Nairobi nchini Kenya. Huanza juu ya Mlima Kenya na ni kijito cha mito Sagana na Tana, mto mrefu zaidi nchini Kenya[2].

Ramani[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Biosafety News, Oktoba / Novemba 2002: Uchafuzi wa Mto Nairobi tisho kwa afya
  2. Rough Guide (2006). Rough Guide Map Kenya [map], 9 edition, 1:900,000, Rough Guide Map. Cartography by World Mapping Project. ISBN 1-84353-359-6.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]