Maji salama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maji salama au maji ya kunywa ni maji yaliyochemshwa au kutibiwa ili yawe salama kwa kunywa au kwa kuandalia chakula.

Kimataifa, katika mwaka 2012, asilimia themanini na tisa (89%) ya watu duniani waliweza kupata maji safi na salama kwa kunywa.

Maji ya bomba ambayo hutumiwa kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani.

Karibu watu bilioni 4 waliweza kupata maji ya bomba wakati wengine bilioni 2.3 waliweza kupata maji kutoka kwenye visima na mabomba ya umma. Watu bilioni 1.8 bado wanatumia maji ya kunywa yasiyo salama ambayo vyanzo vyake vinaweza kuwa vimechafuliwa na kinyesi. Maji haya yanaweza kusababisha magonjwa kama kipindupindu na homa ya matumbo.

Maji ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai wengine. Kiasi cha maji ya kunywa kinachohitajika kinatofautiana. Kinategemea na shughuli za kawaida, umri, masuala ya kiafya na hali ya hewa. Inakadiriwa kuwa Mmarekani mmoja anakunywa lita moja ya maji kwa siku, wakati asilimia tisini na tano (95%) wanakunywa maji yasiyo chini ya lita tatu kwa siku.

Kwa wale wanaofanya kazi katika hali ya hewa ya joto, wanaweza kunywa lita 16 kwa siku. Maji yanatengeneza asilimia sitini (60%) ya uzito kwa wanaume na asilimia hamsini na tano (55%) kwa wanawake. Watoto wachanga wana asilimia sabini (70%) au themanini (80%) ya maji katika miili yao wakati wazee wanakaribia asilimia arobaini na tano (45%).

Kwa kawaida katika nchi zilizoendelea maji ya bomba yanakidhi viwango vya ubora wa maji ya kunywa, hata hivyo kiasi kidogo sana cha maji hayo hunywewa au hutumiwa katika maandalizi ya chakula. Maji hayo hutumika pia katika kufua, usafi wa vyoo na umwagiliaji.

Kupunguza magonjwa yanayosambaa kwa maji na maendeleo ya vyanzo salama vya maji ni lengo kubwa kiafya katika nchi zinazoendelea.

Maji yaliyowekwa katika chupa yanauzwa kwa matumizi ya umma katika sehemu nyingi duniani.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maji salama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.