Tana (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Chanzo cha Tana (picha kutoka Angani)
Tana 1998 wakati wa El Nino
Tana 1998 wakati wa El Nino

Tana ni mto mrefu wa Kenya ukiwa na urefu wa takriban 650 km. Chanzo chake ni milima ya Aberdare magharibi ya Nyeri. Mwanzoni inelekea mashariki halafu ina pinde kuzunguka Mlima Kenya upande wa kusini.

Kisha huingia ndani ya mabwawa ya Masinga na Kiambere yaliyotokana na bwawa la Kindaruma. Chini ya bwawa mto huu hugeuka kuelekea kaskazini na kutiririka mpaka wa kaskazini-kusini kati ya Meru na Kitui Kaskazini na Bisanadi, Kora na Hifadhi ya wanyama ya Rabole. Ndani ya hifadhi hugeuka kuelekea mashariki, na kisha kusini mashariki.

Baadhi ya mito inayoingia mto wa Tana ni mto wa Thika.

Inapita miji ya Garissa, Hola na Garsen kabla ya kufika Bahari Hindi kwenye Ghuba ya Ungwana.