Bungoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bungoma
Bungoma is located in Kenya
Bungoma
Bungoma
Mahali pa mji wa Bungoma katika Kenya
Viwianishi: 0°34′0″N 34°34′0″E / 0.56667°N 34.56667°E / 0.56667; 34.56667
Nchi Kenya
Mkoa Magharibi
Wilaya Bungoma
Idadi ya wakazi
 - 60,650

Bungoma ni mji mdogo katika Kenya ya magharibi karibu na mpaka wa Uganda ambao ni makao makuu ya kaunti ya Bungoma.

Kuna wakazi 60,000.[1]

Bungoma iko kwenye kimo cha mita 1,385 juu ya UB, mguuni pa Mlima Elgon.

Wenyeji wa Bungoma ni Wabukusu ambao ni tawi la Waluhya.

Mji wa Bungoma ulianzishwa kama kituo cha reli ya Uganda katika miaka ya 1920. Bungoma ikateuliwa kama kituo cha mwisho ndani ya Kenya kabla ya kufikia mpaka wa Uganda.

Wakati wa uhuru Bungoma ilionekana kama kijiji kikubwa chenye maduka machache. Mji ukaendelea kukua haraka.

Uchumi umetegemea hasa kilimo kinachostawi vizuri kutokana na hali ya hewa na uwingi wa mvua. Kuna kiwanda cha sukari. Kiwanda cha karatasi cha Webuye kipo karibu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kenya National Bureau of Statistics: Population of local authorities