Wabukusu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wabukusu ni kati ya koo kubwa za Waluhya (Abaluhya) katika magharibi ya Kenya na mashariki-kusini ya Uganda kwenye mitelemko ya mlima Elgon. Eneo lao katika Kenya ni hasa wilaya ya Bungoma (Mkoa wa Magharibi). Wako pia Kitale huko mkoa wa Bonde la Ufa.

Idadi yao ilikadiriwa kuwa karibu lakhi sita mwaka 1987.

Wakati wa kuja kwa ukoloni Wabukusu walijaribu kuwazuia Waingereza. Mwaka 1895 walijitetea katika Boma la Chetambe karibu na Bungoma lakini walishindwa na silaha kali za Waingereza.

Upinzani ulirudiwa katika miaka ya 1940 na 1950 Wabukusu wengi walipomfuata Elijah Masinde na jumuiya yake ya Dini ya Musambwa.

http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=bxk

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabukusu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.