Elgon (mlima)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Eneo la Mlima Elgon

Mlima Elgon ni volkeno inayolala mpakani wa Uganda na Kenya. Kasoko yake ina kipenyo cha kilomita nane.

Elgon ni mlima mkubwa wa pili nchini Kenya baada ya Mlima Kenya. Upande wa Uganda ni mlima mkubwa wa mashariki ya nchi lakini milima ya safu ya Ruwenzori ni kubwa kushinda Elgon.

Jina la mlima limetokana na Waelgonyi walioishi upande wa kusini wa mlima. Wamaasai hutumia jina "Ol Doinyo Ilgoon" na upande wa Uganda huitwa "Masawa".

Kuna vilele vitano:

  • Wagagai (4,321 m), upande wa Uganda
  • Sudek (4,302 m), upande wa Kenya
  • Koitobos (4,222 m), upande wa Kenya
  • Mubiyi (4,211 m), upande wa Kenya
  • Masaba (4,161 m), upande wa Kenya

Mito ya Suam, Nzoia na Turkwell ina chanzo kwa mlima huu. Vilele vya mlima ni sehemu ya hifadhi ya taifa pande zote mbili za Uganda na Kenya.

Miji ya karibu ni Kitale, Bungoma na Webuye upande wa Kenya, halafu Tororo na Mbale upande wa Uganda.