Kaunti ya Nandi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya ramani ikionesha eneo la Kaunti ya Nandi, kenya

Kaunti ya Nandi ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 885,711 katika eneo la km2 2,855.8, msongamano ukiwa hivyo wa watu 310 kwa kilometa mraba[1]. Wenyeji ni hasa wa kabila la Wanandi. Kaunti ya Nandi ni maarufu kwa kuwa nyumbani kwa wakimbiaji wengi, wakiwemo Kipchoge Keino, Henry Rono, Moses Tanui na Bernard Lagat.

Makao makuu yako Kapsabet.

Maumbile ya kaunti hii yanategemea Milima ya Nandi.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Nandi ina maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eeneo bunge Kata
Aldai Kabwareng, Terik, Kemeloi-Maraba, Kobujoi, Kaptumo/Kaboi, Koyo/Ndurio
Chesumei Chemundu, Kosirai, Lelmoko/Ngechek, Kaptel/Kamoiywo, Kiptuya
Emgwen Chepkumia, Kapkangani, Kapsabet, Kilibwoni
Mosop Chepterwai, Kipkaren, Kurgung/Surungai, Kabiyet, Ndalat, Kabisaga, Sangalo/Kebolonik
Nandi Hills Nandi Hills, Chepkunyuk, Chemelil/Chemase, Kapsimatwo
Tinderet Songhor/Soba, Tindiret, Ollessos, Kapchorua

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3][hariri | hariri chanzo]

  • Chesumei 164,133
  • Nandi Central 147,553
  • Nandi East 119,173
  • Nandi North 166,171
  • Nandi South 172,750
  • Tinderet 115,931

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. http://countytrak.infotrakresearch.com/Nandi-county/
  3. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.