Kaunti ya West Pokot

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaunti ya West Pokot
Kaunti
Wanawake Wapokot wakiwa Kapenguria, Pokot Magharibi
Bendera Nembo ya Serikali
West Pokot County in Kenya.svg
Kaunti ya West Pokot katika Kenya
Coordinates: 1°14′00″N 35°07′00″E / 01.23333°N 035.1167°E / 01.23333; 035.1167Coordinates: 1°14′00″N 35°07′00″E / 01.23333°N 035.1167°E / 01.23333; 035.1167
Nchi Kenya
Namba24
IlianzishwaMarch 4, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Bonde la Ufa
Makao MakuuKapenguria
GavanaProf. John Krop Lonyangapuo
Naibu wa GavanaDkt. Nicholas Owon Atudonyang
SenetaSamuel Losuron Poghisio
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Lilian Tomitom
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya West Pokot
SpikaCatherine Mukenyang
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa20
Maeneo bunge/Kaunti ndogo4
Eneo9,123.2 km2 (3,522.5 sq mi)
Idadi ya watu621,241
Wiani wa idadi ya watu68
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutihttp://westpokot.go.ke

Kaunti ya West Pokot ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 621,241 katika eneo la km2 9,123.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 68 kwa kilometa mraba[1]..

Makao makuu yako Kapenguria.

Inajulikana kwa kuwa na bwawa la uzalishaji umeme la pekee lililo kaskazini mwa Bonde la Ufa liitwalo Turkwell. Pia, Makumbusho ya Kapenguria yapo katika kaunti hii, ambapo wapigania uhuru sita walikamatwa na kufungwa jela na serikali ya kikoloni wakati wa hali ya hatari mwaka 1952.

Jiografia

Kaunti ya Pokot Magharibi ina eneo la ukubwa wa 9,169.4 km2 (3,540.3 sq mi). Imepakana na Uganda (magharibi), Turkana (kaskazini), Trans Nzoia na Elgeyo Marakwet (kusini) na Baringo (kusini mashariki).

Kaunti hii ina tabianchi kavu na nusu kavu. Kiwango cha mvua ni kati ya mm 400 hadi mm 1500 kila mwaka. Halijoto huwa kati ya 10 °C na 30 °C[2].

Maeneo bunge

Kaunti ya Pokot Magharibi ina maeneo bunge yafuatayo[3]:

Eneo bunge Kata
Kapenguria Riwo, Kapenguria, Mnagei, Siyoi, Endugh, Sook
Sigor Sekerr, Masool, Lomut, Weiwei
Kacheliba Suam, Kodich, Kasei, Kapchok, Kiwawa, Alale
Pokot South Chepareria, Batei, Lelan, Tapach

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]

  • Kipkomo 102,633
  • Pokot Central 119,016
  • Pokot North 134,485
  • Pokot South 80,661
  • West Pokot 184,446

Tazama pia

Marejeo

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. West Pokot (en-GB). www.crakenya.org. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-07-29. Iliwekwa mnamo 2018-08-05.
  3. West Pokot County | County Trak Kenya (en-US). countytrak.infotrakresearch.com. Iliwekwa mnamo 2018-08-05.
  4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.