Athi River

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Hii ni makala juu ya mji wa Athi River. Angalia pia Mto wa Athi-Galana-Sabaki

Athi River

Athi River ni mji nchini Kenya katika mkoa wa Mashariki uliopo kando la jiji la Nairobi. Inajulikana pia kama Mavoko. Mji huu ni makao ya Baraza ya Mji wa Mavoko na ni mji mkuu wa divisheni ya Mavoko ambayo ni sehemu ya Wilaya ya Machakos. Idadi ya wakazi wa mjini ni 22,000 na jumla ya wakazi ni 48,260 (sensa ya 1999).

Mji huu umeendelea kiasi, ukiwa na pamoja na kiwanda kikubwa cha saruji kinachoendeshwa na kampuni ya Athi River Mining. Mji wa Athi River pia unakua kuwa eneo la makaazi kutokana na ukaribu wake na Nairobi.

Uchukuzi[hariri | hariri chanzo]

Mji huu una kituo cha reli kilicho jengwa mwaka wa 1920 kwenye njia ya reli Mombasa - Nairobi. Chuo Kikuu cha Daystar kina tawi katika mji wa Athi River. Jina la mji huu linatokana na Athi, sehemu ya kwanza ya mfumo wa mto Athi-Galana .

Mji wa Athi River unafuatana na uko kilometa tatu kutoka mji wa Kitengela , lakini ni sehemu ya Wilaya ya Machakos katika Mkoa wa Mashariki, ilhali Kitengela uko kwenye Wilaya ya Kajiado katika Mkoa wa Bonde la Ufa.

Mavoko ilichongwa kutoka kwa Baraza la Mji wa Nairobi mwaka 1963, wakati Baraza la Mji wa Nairobi lilipofutiliwa mbali. Manisipaa ya Mavoko ina wadi sita (Athi River Magharibi, Katani, Kinanie / Mathani, Makadara, Muthwani na Sophia). Zote hizi zimo kwenye eneo bunge la Kathiani, ambayo ina jumla ya wadi kumi. Wadi nne zilizobaki zimo kwenye Baraza ya Mji wa Masaku [1]

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

* Vituo vya reli nchini Kenya

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

[2]* Daily Nation, Aug 21, 2000: Town touched by tragedy

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

* Manispaa ya Mavoko

* FallingRain Map - elevation = 1528m (alama nyekundu ni reli)

[3]

Mji wa Athi River

Wilaya ya Machakos

Majiji,miji na vijiji katika Mkoa wa Mashariki wa Kenya

Mto wa Athi-Galana-Sabaki

[4] [5] [0] ^ ]^ Kenya National Bureau of Statistics: Idadi ya watu wa serikali za mitaa [1] ^ ^ Tume ya Uchaguzi ya Kenya: Usajili wa vituo kwa eneo na eneo la bunge

Anwani ya kijiografia: 01°27′S 36°59′E / 1.45°S 36.983°E / -1.45; 36.983