Athi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Athi ni jina la mto katika Kenya, Afrika. Sehemu za mto hujulikana pia kwa majina ya Galana na Sabaki, kwa hiyo mto wote huitwa pia Athi-Galana-Sabaki.

Ina urefu wa kilomita 390 , na beseni yenye eneo la 70,000 km ².

Mto wa Athi umeupatia jina lake kwa mji wa Athi River karibu na Nairobi pia kwa kampuni ya Athi River Mining.

Athi inaanza karibu na Nairobi ikielekea Bahari Hindi. Inapita Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki pia tambarare ya juu ya Yatta ilipotafuta njia yake kuvukia eneo kubwa la mawe ya kivolkano.

Baada ya maporomoko ya Lugards Falls inapokea mto Tsavo ikibadilika jina lake. Mto unaitwa kuanzia hapa kwa jina la Galana. Kabla ya kufika katika Bara Hindi karibu na Malindi upande wa kaskazini jina linabadilika tena kuwa Sabaki.