Juja

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Juja katika ramani ya Afrika Mashariki.
Juja.

Juja ni mji upatikanao katika kaunti ya Kiambu, kati ya nchi ya Kenya. Mji huu uko katika umbali wa kilometa 36 Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Nairobi. Ni kata ya eneo bunge la Juja[1].

Mji una wakazi 40,446 (sensa ya mwaka 2009[2]).

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Juja ina au mwinuko urefu wa kilometa 700 kutoka juu ya bahari. katika ramani ya dunia, Juja hupatikana katika longitude ya 37 07' 00" na latitude ya -1 11' 00".[3]

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na ripoti kutoka kituo cha utafiti wa hali ya hewa cha Nairobi/Wilson kilichoko umbali wa kilometa 74.8, mji wa Juja una kiwango cha joto cha Nyuzi 24. Upepo huvuma kwa kiwango cha kilometa 23 kwa saa ukielekea Kaskazini Mashariki.

Pia kuna mawingu mepesi katika umbali wa takribani futi 2600 juu ya ardhi.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Juja una taasisi mbalimbali za elimu kuanzia Shule za Msingi, Shule za upili na Vyuo vikuu.

Miongoni mwa taasisi za mafunzo ambazo zimeupa mji wa Juja umaarufu mkubwa ni chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, ambacho kinapatikana huko mjini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]