Kaunti ya Turkana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kaunti ya Turkana
Kaunti
Mto Turkwel ukiwa umekauka wakati wa ukame
Turkana County in Kenya.svg
Kaunti ya Turkana katika Kenya
Coordinates: 3°09′N 35°21′E / 3.150°N 35.350°E / 3.150; 35.350
Nchi Kenya
Namba23
IlianzishwaTarehe 4 Machi 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Bonde la Ufa
Makao MakuuLodwar
Miji mingineLokichogio, Kakuma, Lokichar
GavanaJosphat Koli Nanok
Naibu wa GavanaPeter Lotethiro Emuria
SenetaMalachy Charles Ekal Imana
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Joyce Akai Emanikor
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Turkana
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa30
Maeneo bunge/Kaunti ndogo6
Eneo68,232.9 km2 (26,344.9 sq mi)
Idadi ya watu926,976
Wiani wa idadi ya watu14
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutiturkana.go.ke

Kaunti ya Turkana ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 926,976 katika eneo la km2 68,232.9 msongamano ukiwa hivyo wa watu 14 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Lodwar.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Turkana ndio kaunti kubwa zaidi ikiwa na 71,597.8 km2 (27,644.1 sq mi). Imepakana na Uhabeshi, Sudani Kusini (kaskazini), Uganda (magharibi), Pokot Magharibi, Baringo, Samburu (kusini) na Marsabit (mashariki).

Turkana ina safu za milima: Milima Loima, Milima Lorengippi, Milima Mogila, Milima Songot, Milima Kalapata, Milima Loriu, Milima Kailong’kol na Milima Silale. Safu hizo ni vyanzo vya maji. Vilima vya Tepes, Vilima vya Lokwanamoru, Vilima vya Lorionotom, Vilima vya Pelekech na Vilima vya Loima pia hupatikana katika Turkana[2].

Tambarare za kaunti hupatikana katika sehemu kavu za kaunti.

Mto Tarach, Mto Kerio, Mto Kalapata, Mto Malimalite na Mto Turkwel ndio mito mikuu katika kaunti. Mito hii hupungua kiwango cha maji msimu wa kiangazi, na kukauka wakati wa ukame[3]. Ziwa Turkana liko mashariki mwa kaunti. Limegawanywa kati ya Turkana, Marsabit na Uhabeshi. Katika maeneo karibu na ziwa, kuna chemchemi zilizopo. Chemchemi za Eliye ndio chemchemi maarufu na kivutio cha watalii[2].

Hoteli ya Eliye Springs.

Turkana ina tabianchi kavu na nusu kavu. Kaunti hupata misimu miwili ya mvua: Aprili hadi Julai na Oktoba hadi Novemba[2].

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Turkana imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[4]:

Eneo bunge Kata
Turkana Kaskazini Kaeris, Lake zone, Lapur, Kaaleng/Kaikor, Kibish, Nakalale
Turkana Magharibi Kakuma, Lopur, Letea, Songot, Kalobeyei, Lokichoggio, Nanaam
Turkana Kati Kerio Delta, Kang'atotha, Kalokol, Lodwar Township, Kanamkemer
Loima Kotaruk/Lobei, Turkwel, Loima, Lokiriama/Loren Gippi
Turkana Kusini Kaputir, Katilu, Lobokat, Kalapata, Lokichar
Turkana Mashariki Kapedo/Napeito M, Katilia, Lokori/Kochodin

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [5][hariri | hariri chanzo]

 • Kibish 36,769
 • Loima 107,795
 • Turkana Central 185,305
 • Turkana East 138,526
 • Turkana North 65,218
 • Turkana South 153,736
 • Turkana West 239,627

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
 2. 2.0 2.1 2.2 SECOND ANNUAL DEVELOPMENT PLAN (pdf). Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-01-27. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
 3. Cheboit, Emanuel. Crisis in Turkana as only River dries up - Citizentv.co.ke. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
 4. http://countytrak.infotrakresearch.com/Turkana-county/
 5. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.