Kaunti ya Nyandarua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kaunti ya Nyandarua
Kaunti
Aberdare Ranges.jpg
Flag of Nyandarua County.png Coat of Arms of Nyandarua County.png
Bendera Nembo ya Serikali
Nyandarua County in Kenya.svgNyandarua County in Kenya.svg
Kaunti ya Nyandarua katika Kenya
NchiFlag of Kenya.svg Kenya
Namba18
IlianzishwaTarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa naMkoa wa Kati
Makao MakuuOl Kalou
Miji mingineOl Joro Orok, Kipipiri
GavanaFrancis Thuita Kimemia,EGH, CBS, HSC
Naibu wa GavanaCecilia Wanjiru Mbuthia
SenetaPaul Githiomi Mwangi
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa)Faith Wairimu Gitau
Bunge la KauntiBunge la Kaunti ya Nyandarua
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa25
Maeneo bunge/Kaunti ndogo5
Eneo3,107.7 km2 (1,199.9 sq mi)
Idadi ya watu638,289
Kanda mudaSaa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovutinyandarua.go.ke

Kaunti ya Nyandarua ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 638,289[1].

Makao makuu ya Kanti ya Nyandarua yako kwenye mji wa Ol Kalou.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Nyandarua imepakana na Nyeri, Murang'a (mashariki), Kiambu (kusini), Nakuru (magharibi) na Laikipia (kaskazini).

Iko mashariki mwa Bonde la Ufa ambalo kuumbwa kwake kulisababisha kuwepo kwa safu ya milima ya Aberdare. Milima ya Nyandarua imezungukwa na Mbuga ya Kitaifa ya Aberdare na Hifadhi ya Msitu wa Aberdare[2]. Msitu huo ndio chanzo cha Mto Malewa, Mto Pesi, Mto Turasha, Mto Chania, Mto Kiburu, Mto Mkungi na Mto Kitir[3].

Nyandarua ina Ziwa Ol Bolossat ambalo ni ziwa la pekee katika ukanda wa kati. Kuwepo kwa ziwa hilo kunatishiwa na shughuli za binadamu k.v. ukulima na uchimbaji mawe[4].

Nyandarua huwa na tabianchi baridi na yenye unyevu. Ina misimu miwili ya mvua, Machi hadi Mei na Septemba hadi Disemba[3].

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Nyandarua imegawanywa katika maeneo yafuatayo:

Eneo bunge Wadi
Kinangop Engineer, Gathara, North Kinangop, Murungaru, Njabini/Kibiru, Nyakio, Magumu, Githabai
Kipipiri Wanjohi, Kipipiri, Geta, Githioro
Ol Kalou Karau, Kanjuire Ridge,Milangine, Kaimbaga, Rurii
ol Joro Orok Gathanji, Gatimu, Weru, Charagita
Ndaragwa Leshau/Pondo, Kiriita, Central, Shamata

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. www.knbs.or.ke
  2. The Aberdare Ranges. Iliwekwa mnamo 2018-04-28.
  3. 3.0 3.1 NYANDARUA COUNTY INTEGRATED DEVELOPMENT PLAN Archived Julai 12, 2018 at the Wayback Machine., Ilipatikana mnamo 28/04/2018
  4. Obura, Fredrick. Region's economy under threat as Central Kenya's Lake Ol Bolossat faces extinction :: Kenya - The Standard. Iliwekwa mnamo 2018-04-29.