Kisii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jiji la Kisii
Jiji la Kisii is located in Kenya
Jiji la Kisii
Jiji la Kisii
Mahali pa mji wa Kisii katika Kenya
Majiranukta: 0°41′0″S 34°46′0″E / 0.68333°S 34.76667°E / -0.68333; 34.76667
Nchi Kenya
Mkoa Nyanza
Wilaya Kisii
Idadi ya wakazi
 - 59,248
Tovuti: www.kisii.com

Mji wa Kisii ni mji upatikanao Kusini Magharibi mwa Kenya. Huu ndio mji mkubwa wa kibiashara katika miinuko ya Gusii.

Kisii ndio mji mkuu wa Wilaya ya Kisii Kati. Awali huu ulikuwa makao makuu ya Wilaya ya Kisii kwa ujumla kabla ya wilaya hiyo kugawanwa na kuzaa Wilaya ya Nyamira na Wilaya ya Gucha. Hata hivyo bado mji huu unaendelea kuzifaidi wilaya hizi na Nyanza kusini kwa ujumla, hasa kibiashara.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kuna Shughuli za kiviwanda katika mji huu na vingi vya viwanda hivi vinahusiana na Kilimo kwa kuwa Kisii ni mji ulio katika eneo lililotawalwa na ukulima. Pia kuna uchongaji wa madini katika eneo hili, hasa madini ya soapstone katika eneo la Tabaaka[1].

Elimu[hariri | hariri chanzo]

kutokana na idadi kubwa ya watu na ongezeko la mahitaji ya kielimu, vyuo vingi vimeanzisha matawi yao nchini Kisii. Miongoni mwa vyuo vilivyoanzisha matawi yao mjini ni:

Licha ya hayo kuna shule nyingi za Sekondari humo mjini, miongoni mwao zikiwa:

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mji huu una wakazi wa matabaka mbalimbali miongoni mwao wakiwa Wahindi na Wakikuyu wanaojihusisha na biashara, huku idadi kubwa ikiwa Wakisii.

Hata hivyo, Wahindi wamenunua mali nyingi kutoka kwa Wakisii, ambayo wamekuza kuwa maduka makuu na jambo hili limeukuza mjii huu kiajabu hivi karibuni. Leo hii mji huu unajivunia maduka makuu kama Tuskys na Nakumatt, benki kuu kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, K-Rep, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays ambayo yote yameanzisha matawi mjini Kisii.

Hali ya Usafi na Nyumba[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Kisii una kiwango cha chini cha usafirishaji wa takataka na maji machafu. Kituo pekee cha kusafisha maji machafu kilikuwa Daraja Mbili lakini kimehamishwa nje ya Mji. Mji huu pia unakumbwa na uhaba wa ardhi huku mitaa mingi mjini ikianzishwa bila mpango maalumu.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tabaka la Kisii (Kisii Tribe)-Carvers of Soapstone in Kisii: kenya-information-guide.com
  2. Egerton University, Kisii Campus:Egerton University Website

0°41′S 34°46′E / 0.683°S 34.767°E / -0.683; 34.767