Shule ya Upili ya Kisii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shule ya Kisii


Shule ya Upili ya Kisii ni shule maarufu na ya kitambo. Shule hii inapatikana katika Mji wa Kisii, Wilaya ya Kisii, Mkoani Nyanza nchini Kenya.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ilianzishwa mnamo 1932 na muungano wa Young Kavirondo Association. Ilikuwa moja kati ya Shule tatu za K zilizoanzishwa na Waafrika wakati wa Ukoloni. Shule hizi ni:

Shule hizi tatu ziliitwa Government African Schools (G.A.S).

Kuihusu shule hii[hariri | hariri chanzo]

Shule hii imekuwa na uunganishi mkubwa na Familia ya Musa Nyandusi ambaye alikuwa Chifu wa Kiwango cha juu wakati wa Ukoloni. Cheo hiki kilikuwa cha nguvu na kilikuwa tu kinapokea amri kutoka kwa Utawala wa Ukoloni pasipo na uchungaji Shule hii inajuvunia kuwakuza watu maarufu kama Simeon Nyachae, Mwanaye Musa Nyandusi. Sasa hivi shule hii inahesabiwa kama taasisi muhimu ya masomo katika nchi, ambayo inaweza kushindana na shule za kataifa katika mtihani wa K.C.S.E. ilivyoonekana mnamo 2005 wakati shule hii ilitia fora.

Mwito wa Shule[hariri | hariri chanzo]

Mwito wa Shule hii ukitafsiriwa kwa kiswahili unakuwa: Ng'ang'ana Kutia fora' (Strive for Excellence)

Soka ya Shule[hariri | hariri chanzo]

chini ya uongozi wa Joseph Kinaro, mwalimu mkuu aliyeondoka, Kisii iliibuka timu bora zaidi ya Shule katika soka mnamo miaka ya tisini. Rekodi waliyoiweka inaweza kushindaniwa tu na timu ya Shule ya Kakamega. Walishinda makombe matatu ya Kitaifa mfululizo mnamo 1996- 1999. Wengi wa wachezaji wake wameichezea Timu ya Taifa, na baadhi ya wengine anacheza soka ya kulipwa barani Uropa na Asia.

Utata[hariri | hariri chanzo]

shule hii ilikumwa na madai ya udanganyifu katika mtihani na hivyo Watahiniwa wengi wa mwaka wa 2006 wakapata alama ya Y. Tukio hili lilitia kitone historia yao nzuri ya kielimu.

Watu maarufu waliosoma huko[hariri | hariri chanzo]

Mafanikio ya Shule hii yanatarajiwa kuimarishwa na wakongwe wa Shule hii, baadhi yao wakiishi Uropa na Marekani.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Shule ya Upili ya Kisii kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.