Nakumatt
Nakumatt ni mtandao wa maduka nchini Kenya. Ina maduka 18 kote nchini Kenya na inaajiri watu 3,200. Ina mipango ya kupanua maduka yake mpaka nchini Uganda, Rwanda na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Nakumatt ni kampuni ya Kenya inayomilikiwa na familia na Atul Shah Hotnet Ltd.[1] [2]
Mnamo 23 Agosti 2008, Nakumatt ilifungua ghala yake ya kwanza nje ya Kenya katika Union Trade Center, mjini Kigali, Rwanda.[3]
Mauzo ya mwaka 2006 ilikuwa zaidi ya US $ 300m, iliyozidi kwa 150% ya mauzo ya mwaka uliopita.[4] Kampuni hii ilikuwa na madai ya kushiriki katika ukwepaji wa kulipa ushuru mwaka 2006, ingawa hadi sasa hakuna mashtaka yaliyopelekwa kortini.[5] Nakumatt ni ufupisho wa Nakuru Mattresses.[6]
Ghala moja ya Nakumatt mjini Nairobi ilichomeka kwa moto mkubwa mnamo 28 Januari 2009, na kuua watu 25.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Afrika Mashariki 25-31 Agosti 2008 - Special Supplement
- ↑ "Nakumatt Prepares to Sell In Rwanda", AllAfrica, 11 Juni 2007. Retrieved on 2007-06-13.
- ↑ http://allafrica.com/stories/200808250206.html
- ↑ "Nakumatt Turnover grows by 150%", AllAfrica, 30 Mei 2007. Retrieved on 2007-06-13.
- ↑ "Nakumatt Chain Probed Over Tax Queries", East African Business Week, 10 Aprili 2006. Retrieved on 2007-06-13.
- ↑ "Kenya: Nakumatt to Be Listed At NSE, Says Director", The Nation, 5 Oktoba 2007. Retrieved on 2007-12-07.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi ya Nakumatt Ilihifadhiwa 20 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nakumatt kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |